• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

NMB MKALAMA KUADHIMISHA HUDUMA KWA WATEJA KWAKUBORESHA HUDUMA ZA NMB MKONONI

Imewekwa kwenye: October 5th, 2022

Benki ya NMB  tawi la Mkalama leo  imeungana na  Duniani  nzima  kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa  kila mwaka  kwa wiki ya kwanza ya  mwezi  Oktoba.

Akiongea katika maadhimisho hayo  Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri ya wilaya ya Mkalama ambaye alikua  mgeni  rasmi katika hafla hiyo Bi. Asia Messos aliwataka  wananchi  pamoja  na wadau  mbalimbali  kuendelea kuiamini na kutumia benki ya NMB  katika huduma za kifedha.

Aidha Bi. Messos  alisema kama serikali wataendelea kuuunga mkono juhudi  zote zinazofanywa na BENKI hiyo  katika kuboresha huduma za  kifedha  wilayani  hapa huku akiwataka wadau wa maendeleo na watumiaji  wa  Benk i ya  NMB kutumia wiki hii ya huduma kwa wateja kutoa maoni na mapendekezo mbalimbali juu ya kuboreshwa kwa huduma kama ilivyo kwakauli mbiu  isemayo NMB  karibu yako.

Pia aliwapongeza  wafanyakazi  wa  benki hiyo kwa huduma bora wanazotoa wilayani  Mkalama na kuwataka kuendelea  kuboresha zaidi ili  kuendea kuaminiwa na watumiaji wa Benki hiyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Meneja wa Benki ya NMB  huduma kwa teja wilaya ya Mkalama Bw. Emmanuel  Gambalagi   alisema kuwa wanatambua umuhimu wa  kubuni na kufanya maboresho zaidi kwenye  huduma hususani zile za kidigitali ili kurahisisha  huduma  kwa wateja.

‘’Tunashuku na tunaendelea kuwa karibu na  wateja  wetu  ili kuishi kauli mbiu yetu ya ‘NMB KARIBU YAKO’ na  nitumie fursa hii kuwahakikishia watanzania kuwa benki ya NMB  itaendelea kuja na masuluhisho bora  inayotokana na ubunifu wa kidigitali yenye kurahisisha zaidi huduma za kifedha’’ alisema  Bw. Gambalagi

Aidha aliongeza kuwa  katika maadhimisho ya mwaka huu wanatangaza maboresho  katika huduma mbili zilizopo kwenye NMB mkononi ambazo ni  Mshiko  Fasta  na  Spend to Save.

‘’Spend  to save ni huduma inayomsaidia mteja kujiwekea akiba kulingana na matumizi yake na Mshiko Fasta ni huduma inayompa fursa mteja kukopa fedha kupitia simu yake ya mkononi  bila dhamana wala kufika matawini.’’ Aliongeza  Gambalagi Meneja huduma kwa wateja

Akiongea kwa niaba ya wateja wa Benki hiyo wilayani Mkalama Bw. Alfred Msengi  aliipongeza kwa huduma bora wanazotoa kwa wateja na kuahidi kuendelea kuunga mkono na kutumia Benki ya NMB kutoka na huduma zake kufika kila mahali na kuwa karibu na wateja wao.

Maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Wateja hufanyika kila  ifikapo wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba na  kwa mwaka huu  huu ilianza Oktoba 3 na kufikia kilele Oktoba 7 huku kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni ‘’Sheherekea Huduma’’. ( Celebrate Service).

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.