Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Mosses Machali ameipongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA) Wilaya ya Mkalama kwa kuongeza usajili wa Wafanyabiashara wapya wapatao 477 pamoja na kuvuka lengo la ukusanyaji wa Mapato kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo walikusudia kukusanya Milioni 250 lakini wakakusanya Milioni 277 na mwaka 2022/2023 kukusanya Milioni 700 hadi kufikia leo Mei 31 2023 wamekusanya Milioni 611.
Ametoa pongezi hizo katika kikao cha Kamati ya Ushauri wa Kodi Wilaya ya Mkalama yenye lengo la kupitia utendaji wa kazi wa Mamlaka ya Mapato Wilaya inayojumuisha Wafanyabiashara mbalimbali wanaochangia na kutoa dira juu ya hali ya biashara na ukusanyaji mapato Wilayani hapa.
‘’Niwapongeze ‘TRA’ kwa ukusanyaji wa mapato na kuvuka lengo mlilojiwekea kutoka mwaka 2021/2022 na kwa mwaka 2022/2023 ambapo hadi sasa mmekusanya Milioni 611 na hapa Meneja katuambia hadi kufika june 30 mtakuwa mmevuka lengo’’ Aliongeza Mhe. Machali.
Mhe. Machali amesisitiza ushirikiano baina ya Mamlaka ya Mapato, TARURA, Halmashauri ya Wilaya pamoja na Taasisi zote Wilayani hapa ili kuongeza ukusanyaji wa mapato Wilayani pamoja na kuitaka Kamati kuhakikisha kila mmoja kwa nafasi yake anasimamia suala hilo kikamilifu kwa maendeleo ya ya wananchi.
Awali akiwasilisha taarifa Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Mkalama CPA. Iddi Omary amesema kuwa kwa kushirikiana na Halmashauri na TARURA wanatarajia kuongeza ukusanyaji na kuvuka lengo walilojiwekea la kukusanya Sh. Milioni 700 kwa 2022/2023 huku akiongeza kwa mwaka wa fedha 2023/2024 wamejipanga kukusanya sh 1.5 Bilioni.
Pamoja na hayo CPA Omary aliongeza kwakusema TRA Wilaya pamoja na kutoa mafunzo ya kuwajengeza uwezo Kamati pamoja na kuendelea kutumia mashine za Kielekitroniki (EFD) katika kutoa risiti ili wananchi waendelee kufurahia huduma iliyobora Zaidi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.