• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Nitafuatilia daraja hili usiku na mchana-Magufuli

Imewekwa kwenye: September 10th, 2018



“Haiwezekani  ujenzi wa daraja uchukue zaidi ya miaka sita wakati mkandarasi analipwa stahiki zake zote kwa wakati tena kwa kutumia kodi za Watanzania hivyo daraja hili ni lazima likamilike ifikapo mwezi machi mwakani, Wizara mjipange kweli kweli kwa sababu tutafukuzana hapa hapa na kuanzia sasa hivi nalifanya kuwa kipaumbele changu namba moja kwa kulifuatilia hivyo ntapiga simu usiku na mchana ili kujua limefikia wapi”

Ni kauli iliyotolewa mapema leo na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Daktari  John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi la Mto Sibiti baada ya  kutofurahishwa na kasi ya mkandarasi anayejenga daraja la mto huo  huku pia akizikataa sababu mbalimbali za uchelewaji huo zilizotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa wakala wa barabara wa Taifa (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe. Isack Kamwelwe.

“ Waziri kama unaona mkandarasi huyu hana uwezo wa kumaliza kazi hii kwa wakati ni bora utafute mkandarasi mwingine kwa sababu sina uhakika hata kama mkandarasi huyu ana vifaa vya kutosha kumaliza kazi hii na huenda hata hivi navyoviona hapa vimeletwa jana usiku baada ya kusikia ninakuja leo” Aliongeza Mhe. Magufuli.

Mhe. Magufuli aliwaagiza wenyeviti wa bodi ya wakandarasi na washauri wa wakandarasi kuwasimamia ipasavyo mkandarasi na mshauri wa mkandarasi  wa daraja hilo na kama wataonekana kufanya kazi chini ya kiwango wachukuliwe hatua kwa mujibu wa taratibu za bosi hizo.

“Nyie ‘consultants’  mnapaswa kujua mpo hapo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na najua nyie ni wafanyabiashara but this is not a good business for you  so watch out’’ Alionya Mhe. Magufuli.

Katika hotuba yake Mhe. Magufuli aliieleza halaiki ya wananchi waliojitokeza katika tukio hilo kuwa baada ya kukamilika kwa daraja hilo  uchumi wa Mikoa ya Singida na Simiyu utaimarika zaidi kwa sababu utawapa fursa wananchi wa pande hizo mbili kufanya biashara ya rasilimali wanazozalisha.

“Waziri wa Madini amesema hapa kuwa Mkoa wa Simiyu una chumvi nyingi sana kwa hiyo nategemea kukamilika kwa daraja hili kutachochea uchimbaji zaidi wa chumvi hiyo ambapo kiwango kikiridhisha tunaweza hata kuongeza kodi ya uingizaji wa chumvi ya nje ili kuongeza matumizi ya chumvi tunayozalisha wenyewe hapa ndani” Alisisitiza Mhe. Magufuli.

Mhe. Rais alihitimisha hotuba yake kwa kumpongeza Mbunge wa Mkalama Mhe. Allan Kiula kwa ushirikiano mzuri alionao dhidi ya wanasiasa wenzake ndani ya Wilaya na wataalam wote wa Wilaya hiyo ambapo alimtaka kuendeleza ushirikiano huo ili kuzidi kuongeza maendeleo ya Wilaya hiyo.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Daktari Rehema Nchimbi alimshukuru Mhe. Magufuli kwa ujenzi wa daraja hilo ambapo alimhakikishia kuwa tayari Mkoa wa Singida umejipanga kuhusu matumizi sahihi ya daraja hilo na mkakati wa utunzaji wa mazingira yanazunguka daraja hilo umeshakamilika.

“Mhe. Rais ninakushukuru kwa sababu hivi sasa maji ya ziwa Victoria yatakayopita Simiyu yatafika mpaka Singida kupitia Mkalama” Alisema Mhe. Nchimbi.

Mpaka sasa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetumia zaidi ya shilingi bilioni 2002 za mapato yake ya ndani katika kuboresha na kutengeneza miundombinu ya barabara huku daraja la Sibiti likigharimu jumla ya shilingi bilioni 16 mpaka kukamilika kwake ambapo kwa sasa limefikia asilimia 70 na kugharimu shingi bilioni 15.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.