• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Ni lazima tuwe na fikra na uongozi wa kimkakati- Nchimbi

Imewekwa kwenye: September 14th, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Daktari Rehema Nchimbi amelaani kitendo cha Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi na watu wasiofahamika akiwa kwenye gari yake kilichotokea hivi karibuni akiwa kwenye gari nyumbani kwake Dodoma.

Mhe. Nchimbi amelaani tukio hilo muda mchache kabla ya kufungua  kikao cha  Umoja wa mamlaka ya serikali za mitaa (ALAT) ngazi ya Mkoa wa Singida huku ikiwa ni mara yake ya kwanza kuzungumza hadharani kuhusiana na tukio hilo tangu kutokea kwake.

“Bila kujali itikadi za kisiasa, dini au kabila, suala lililomtokea Mhe. Tundu Lissu linapaswa kulaaniwa na kila Mtu hasa sisi wa Mkoa wa Singida kwa sababu ni Mbunge anayeutumikia Mkoa wetu na ni mwananchi mwenzetu wa Mkoa wa Singida” Alisema Mhe. Nchimbi.

Mhe. Nchimbi amesema kuwa ni vizuri Wananchi wote wa Mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla wawe na subira na Imani dhidi ya vyombo vya Ulinzi na Usalama ambavyo bado vinaendelea kulifuatilia na kuchunguza  tukio hilo kwa ukaribu.

“Si jambo jema kumnyooshea kidole mtu, kundi la watu au taasisi fulani kuhusiana na tukio hili kwa sababu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vipo makini sana na baada ya kumaliza kazi yao vitatoa majibu sahihi yaliyotokana na uchunguzi wao hivyo kwa sasa tuwe na subira na tuungane kumuombea ndugu yetu Mhe. Lissu aweze kupona na kurejea katika majukumu yake ya kuwahudumia Watanzania” Alisisitiza Mhe. Nchimbi.

Katika kikao hicho Mhe. Nchimbi amewataka viongozi wote wa halmashauri za Mkoa wa Singida kuwa na fikra  na uongozi wa kimkakati ili kuhakikisha wanawahudumia wananchi wote kutokana na rasilimali zilizopo bila kujali zinatosha au la.

“Kama utakuwa na ‘strategic thinking’ maana yake utakuwa na uwezo wa kujua namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wako kulingana na rasilimali ulionazo na kamwe huwezi kuwa na kisingizio kuwa miundombinu haijitoshelezi” Alisema Mhe. Nchimbi.

Mhe. Nchimbi amesema baada ya kuwa na fikra za kimkakati ni lazima viongozi wote wa Wilya husika wawe na uongozi wa kimkakati ambao utampa nafasi kila kiongozi kwa nafasi yake kutoa mchango wake katika kutatua changamoto za wananchi.

“Sio unaenda Ofisini kwa Mkuu wa Wilaya na kumueleza tatizo lako anasema mimi ni ‘DC’ kwa hiyo kama ni ‘DC’  ‘so what’, ni lazima katika kila changamoto ya mwananchi mchango wa kila kiongozi uonekane” Alisisitiza Mhe. Nchimbi.

Mhe. Nchimbi alihitimisha hotuba yake fupi kwa kuwataka viongozi wanaounda umoja huo Mkoani Singida kuhakikisha wanaifanya Singida kuwa Mkoa wa Viwanda kwa kuwavuta wawekezaji wengi zaidi kuchangamkia fursa nyingi zilizopo Mkoani hapa.

“Kuna ngozi nyingi sana inatoka mkoani Singida, hebu jaribuni kuangalia namna gani tunaweza kuanzisha kiwanda cha ngozi hapa na pia naomba nyie mshiriki katika Kilimo cha mazao mbalimbali yanayostawi vizuri Mkoani Singida huku mkisisitiza na wananchi nao kufanya hivyo na hatimaye tuongeze uzalishaji wa mazao yanayoupa sifa kubwa mkoa wa Singida” Alimalizia Mhe. Nchimbi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.