Ametoa maagizo hayo mapema leo katika ukumbi wa Sheketela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambao pia ulihususisha viongozi wa taasisi mbalimbali na dini ambao aliwata kila mmoja kwa nafasi yake kusimamia suala hili ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
Mhe. Machali amesema kuwa ugonjwa wa kipindupindu unasababishwa na uchafu wa mazingira ikiwepo kaya nyingi wilayani hapa kukosa vyoo bora hivyo kuwaagiza Watendaji hao kuanzia kesho novemba, 09, 2023 kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao ili wananchi wapate elimu ya usafi wa mazingira pamoja na kuwa na vyoo bora.
‘’Maelekezo yangu ni kwamba nendeni kwenye maeneo yenu wewe Mwenyekiti wa kijiji ,mtendaji wa kijiji, Kata mkahakikishe ndani ya siku 10 kila kaya inakuwa na choo bora natoa maelekezo kuwachukulia hatua kali za kisheria watakao puuza agizo hilo’’ Alisisitiza Mhe.Machali.
Pamoja na hayo aliwataka viongozi wa dini wanapokuwa kwenye nyumba zao za ibada kutoa elimu kwa waumini wao kuhusu hatari kuwepo kwa maambukizi ya ugonjwa huu hatari wa mlipuko na kuwataka kuchukua tahadhari zote za kiafya katika kuzuia maambukizi hayo kuenea katika maeneo mengine.
Aidha ameagiza kuwepo kwa vyoo katika maeneo yote ya taasisi za umma, mashirika ya dini, soko, shuleni, stendi ya mabasi , nyumba za ibada na kwenye mikusanyiko kuwepo vifaa vya kunawia mikono ikiwepo sabuni na vitakasa mikono ambapo amewataka wananchi kuacha kusalimiana kwakutumia mikono ili kuzuia maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Sanjari na hayo amemuagiza Meneja wa Wakala wa maji na usafi wa mazingira Wilaya ya Mkalama( RUWASA) kuchukua sampuli za Maji pamoja na kutibu visima virefu na vifupi ndani ya Wilaya ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kutapika na kuharisha ( KIPINDUPINDU).
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.