Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dr. Sweetbert Zakaria Mkama amewataka wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama kumsaidia Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza usalama wa chakula unakamilika kwa wakati.
Ameyasema hayo Oktoba 24 mwaka 2022 wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Mkalama yenye lengo la kukagua mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza Usalama wa Chakula katika maeneo kame.
Aidha, aliongeza Wananchi wanahitaji huduma karibu na maeneo yao kama vile maji, Shule na huduma zingine hivyo kuwataka wanaohusika na manunuzi kuhakikisha kwenye maeneo ya mradi wanafanya manunuzi mapema ili wananchi wapate huduma katika kuunga mkono juhudi za Serikali ambayo inatoa fedha nyingi ili kupeleka miradi kwa jamii.
‘’Niwatake wakuu wa Idara na Vitengo kila mmoja kwa nafasi yake kusimamia wajibu wake ili kuhakikisha fedha zinazotolewa na Serikali zinazaa matunda kwa wananchi ‘’ Aliongeza Dr. Mkama.
Katika ziara yake alikagua mashine mbili za kukoboa mpunga na kutaka zipelekwe mapema kwa wananchi kabla ya mvua kuanza na kuagiza ukamilishwaji wa majengo kwa ajili ya kufunga mashine .
Mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza Usalama wa Chakula unatekelezwa katika Vijiji vitano (5) vya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Nyahaa, Mkiko, Lugongo , Mpambala pamoja na Kijiji cha Munguli
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.