Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Mhe. James Mkwega,amewapongeza wananchi wa Kijiji cha Nkenke pamoja na viongozi wa eneo hilo kwamoyo wao wa kujitolea uliowezesha kukamilika kwa ujenzi wa zahanati ya kijijihicho, hatua ambayo sasa imewarahisishia upatikanaji wa huduma bora za afyakaribu na makazi yao.
Mhe. Mkwega ametoa pongezi hizo Juni 13,2025wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa zahanati hiyo iliyofanyika leo katikaKijiji cha Nkenke, Kata ya Kikhonda.
"Niwapongeze wananchi wa Nkenke kwa juhudizenu kubwa mlizozionesha hadi kufanikisha ujenzi wa zahanati hii. Kuanzia sasa,hakuna tena haja ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma Ishenga, Kikhonda auKinampundu. alisema Mhe. Mkwega kwa msisitizo.
Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Wilaya yaMkalama, Dkt. Solomon Michael, amesema kuwa katika kipindi cha mwaka mmojapekee, zaidi ya zahanati 11 zimezinduliwa na kuanza kutoa huduma kwa wananchi,akitaja hatua hiyo kuwa ni mafanikio makubwa katika sekta ya afya.
Baadhi ya wananchi waliokuwepo katika hafla hiyo wameishukuru Serikali yaAwamu ya Sita kwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya katika Kijiji chaNkenke, wakieleza kuwa awali walilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata hudumakatika vijiji jirani.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.