Jumla ya vyumba vya madarasa ya shule za msingi za Serikali elifu 12 (12,000) vinatarajiwa kujengwa Katika maeneo yenye Upungufu au msongamano wa wanafunzi kupitia mradi mpya wa BOOST unaotekelezwa kwa gharama ya Tsh. Triilioni 1.15 nchi nzima
Kauli hiyo imetolewa Desemba 13 2022 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angela Kairuki wakati akifungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa timu za utekelezaji wa Mradi wa BOOST ngazi ya Mkoa na Halamashauri Uliofanyika Katika ukumbi wa mikutano uliopo Katika shule ya sekondari ya Iliboru Mkoani Arusha.
Kairuki amesema Serikali imeendelea kujenga vyumba vingi vya madasa ya Sekondari ambapo imesaidia kuondoa changamoto ya msongamano na kwamba kwa sasa Serikali kwa kushirikiana na Benki ya dunia imeanzisha Mradi huo wa BOOST Ili kutatua Changamoto zinazoikabili elimu ya awali na msingi Nchini kote.
"kupitia Mradi huu, Serikali itajenga na kukarabati miundombinu ya shule za awali na msingi. Naipongeza serikali kwa Kuanzisha Mradi wa miaka mitano wa kuimarisha ubora wa elimu ya awali na Msingi (BOOST) ambapo katika kipindi hicho, jumla ya shilingi trilioni 1.15 zitatumika" Alisema Kairuki.
Aidha amezitaja changamoto nyingine zitakazotatuliwa na mradi huo ni
baadhi ya shule kutokuwa na mazingira rafiki ya kufundishia na kujifunzia kama vile uwepo wa miundombinu chakavu,
Upungufu wa vyumba vya madarasa unaosababisha msongamano wa wanafunzi darasani,
baadhi ya wanafunzi wanamaliza Darasa la Kwanza na la Pili bila kumudu stadi za KKK(kusoma, kuandika, na kuhesabu) na kumaliza darasa la Saba bila umahiri wa somo la Kiingereza.
Aidha ameeleza kwamba Upungufu wa vifaa visaidizi kwa ajili ya kuwezesha ujifunzaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum; na
Upungufu wa vifaa na matumizi ya TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji ni sehemu ya Changamoto zitakazotatuliwa na utekelezaji wa Mradi huo unaotekelezwa kwa kuzingatia matokea.
Hata hivyo Kairuki amesema kwamba OR-TAMISEMI imefanya tathmini ya hali halisi ya miundombinu ya uchakavu kwa Shule zote za Msingi za Serikali zipatazo 17,182 nchi nzima ambapo Matokeo ya tathmini yameonesha kuwa, shule za msingi 1,804 sawa na asilimia 6.3 zina msongamano mkubwa wa wanafunzi.
Waziri ameendelea ameendelea kueleza kwamba vyumba vya madarasa vipatavyo 7,741 kati ya 147,284 sawa na asilimia 5 vinahitaji kubomolewa na kujengwa upya, wakati madarasa 35,914 sawa na asilimia 24 yanahitaji ukarabati mkubwa.
Akimalizia hotuba yake Waziri huyo ameeleza kwamba tathmini hiyo imebaini uwepo wa vijiji au mitaa 1,544 ambayo haina shule za Msingi hivyo kusababisha wanafunzi wa shule za msingi na Awali kukosa Huduma hiyo muhimu.
Wakati huo huo, Kairuki ameagiza halmashauri zote kuhakikisha wanaandikisha watoto wote wenye umri wa kuanza shule za awali tayari Kwa kujunga na elimu hiyo Januari 2023.
Mkutano umewakutanisha jumla ya Maafisa 226 Kutoka ngazi za Mkoa na Halmashauri ikihusisha Maafisa elimu msingi, Maafisa habari, wagavi ngazi ya Halmashauri wahandisi na Maafisa Maendeleo ya jamii. Wengine ni maafisa Ustawi wa jamii, waweka Hazina wa Halmashauri, Maafisa elimu Kata, walimu wakuu na waratibu wa mradi wa BOOST.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.