Jamii imetakiwa kujua na kuelewa haki zao za Msingi Ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza kwa kukosa uelewa wa mahala sahihi katika kuwasilisha changamoto zao na kupatiwa msaada wa masuala mbalimbali ikiwemo migogoro ya Ardhi, Ndoa pamoja na haki zingine kama vile ya kuishi na kuheshimiwa katika kutoa mawazo.
Hayo yamesemwa Januari 17 , 2024 na Wakili wa Serikali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Daud Makendi katika Mkutano wa hadharani wa Wananchi wa vijiji vya Malaja Kata ya Nkalakala, na Mazangili Kata ya Nkinto, katika Kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia Suluhu ( Mama Samia Legal Aid Campaign).
Aidha, amewataka Wananchi kuacha kujichukulia Sheria mkononi kama njia ya kupata Suluhu kwao kwani kwa kufanya hivyo itapelekea wao kupoteza haki za Msingi na kukosa haki aliyostahili kuipata.
Pia Wakili, Makendi amewaeleza Wananchi hao Mamlaka za utatuzi wa migogoro ya Ardhi kuwa ni Baraza la Ardhi la Kata, Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa.
Pamoja na hayo Wakili Makendi aliwataka Wananchi kuandika Wosia ili kuwasaidia wanaobakia kuendelea kutumia Mali alizoziacha muhusika na kuepusha migogoro ya kunyang'anywa Mali na watu wasiokuwa warithi.
" Msiogope kuandika wosia , kwa kudhani mnajichuria kifo" Alisisitiza
Sanjari na hayo amesisitiza kuwa faida za kuandika Wosia ni kuwapa haki wanaostahili kupata mgawanyo wa Mali ulizonazo ambapo ameongeza kwa kusema kuwa kwa mujibu wa Sheria wanaoruhusiwa kurithi Mali hizo ni wahusika wa familia ambao ni Mjane/ Mgane pamoja na watoto
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.