Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machari amewaomba Wananchi wa Wilaya ya Mkalama , Watumishi wa Idara na Vitengo Pamoja na Taasisi zote Wilayani hapa kumpa ushirikiano wa kutosha ili kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya , Mhe. Sophia Kizigo kuhakikisha Wilaya inasonga mbele zaidi kimaendeleo.
Ameyassema hayo mapema leo February 4, 2023 wakati wamakabidhiano ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, ambapo amesema kuwa anamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kumuamini kwa kipindi kingine na kumteua kuja kuitumikia Wilaya ya Mkalama akitokea Wilaya ya Bukoba na kuahidi kufanya kazi kama timu kwa masilahi mapana ya Wilaya ya Mkalama.
‘’Awali ya Yote ninamshukuru Mwenyezi Mungu kutukutanisha leo, Lakini pia Shukrani zangu zimwendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kuona ninafaa kuja kuitumikia Wilaya ya Mkalama , kubwa ninaomba ushirikiano wenu kwasababu kutekeleza majukumu haya ni ‘connection’ , sijaja kutangua torati bali nimekuja kuendeleza yale mazuri yaliyofanywa na Mhe.Kizigo’’ Aliongeza Mhe. Machari.
Aidha alisema kuwa atahakikisha analinda Imani iliyojengwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo kwa Wananchi wa Mkalama huku akiwataka watumishi wote kila mmoja kwa nafasi yake kufanya majukumu yake kikamilifu ili kuepuka migongano katika utendaji kazi .
Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo amewashukuru watumishi wote wa Wilaya ya Mkalama, Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ,Mwenyekiti wa Halmashauri, Baraza la Madiwani Pamoja na Taasisi zote Wilayani hapa kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi chote akiwa Wilayani Mkalama na kuwaomba kumpa ushirikiano huo Mhe . Machari ambaye ndio Mkuu wa Wilaya .
Pamoja na hayo Mhe. Kizigo amemkabishi Ofisi Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Machari nakumwambia Mkalama iko salama na watu wake ni wachapa kazi na wanaendelea na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwa ni Pamoja na Kilimo, Ufugaji na shughuli za uchimbaji wa madini hivyo kumuomba kuendeleze alipoishia na kuibua mengine mapya kwa ustawi wa Wilaya ya Mkalama.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.