Mkoa wa Singida unajivunia mapinduzi katika sekta ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara ikiwa leo ni maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wa Tanganyika uliopatikana mwaka 1961 chini ya baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Evodius Katare amesema hayo katika hutuba yake wakati wa maadhimisho ya uhuru ambayo yamefanyika kimkoa katika Wilaya ya Mkalama amesema kuwa Kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1970 mkoa wa Singida haukuwa na uzalishaji toshelevu wa mazao ya chakula na hata ya Biashara kabla ya maboresho ya teknolojia na dhana za kilimo jambo liliopelekea kuwa tegemezi na kuwafanya wananchi kuanza kuomba misaada kwa serikali.
"Miaka 61 ya uhuru uzalishaji umeongezeka na kuifanya singida kuwa na chakula cha kutosha ambapo uzalishaji umeongezeka kutoka tani 197886 mwaka 1990 hadi tani 649850.02 mwaka 2021 /2022 ongezeko hilo likitokana na jitihada za kuongeza uzalishaji kwa mkoa huu ambao ulikuwa ni miongoni mwa mikoa ambao ilikuwa inategemea misaada ya chakula"".Alisema Katare.
“Mkoa wa Singida ulikuwa ni Miongoni mwa mikoa ambayo ilikuwa na uhaba wa chakula mpaka ikafikia hatua wananchi wakawa wanaomba serikali iwapatie msaada lakini katika miaka 61 ya uhuru kumekuwa na mabadiliko makubwa katika teknolojia na dhana za kilimo jambo ambalo limeongeza uzalishaji wa mazao ya chakula”, Alisema Katare.
Awali Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Messos alitoa salamu za watumishi wa Mkalama alisitiza juu ya uwajibikaji katika kutimiza majukumu ya kila siku kwa watumishi na wananchi kwa ujumla ambapo alisema kuwa kila mtumishi ni lazima awajibike katika majukumu yake na hapaswi kuona ugumu kuwajibika katika utendeji wake.
Aidha aliendelea kutoa mfano kitendo cha aliye kuwa Rais wa awamu ya Pili mzee Ali Hassani Mwinyi cha Kujiuzuru kuwa ni moja ya uwajibikaji na kuwa sio kosa kufanya hivyo pale unapolazimika kufanya .
“Ili tuweze kuwa na maendeleo lazima ndugu zangu watumishi wenzangu tuwajibike kwa kwa kuwajibika tutaweza kutimiza majukumu yetu hivyo uwajibikaji kwetu ni lazima hasa katika kuwahudumia wananchi”,Alisema Mesos.
Aidha aliwataka wananchi wa Mkalama kushiriki na kuunga juhudi za serikali zinazoendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali na sekta tofauti na kuongeza kuwa kupatikana kwa Wilaya ya Mkalama kumerahisisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, kilimo , Miundombinu na umeme huku uwepo wa ofisi za kiserikali karibu na wananchi kumerahisha upatikanaji wa huduma karibu na makazi ya watu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama James Mkwega alisema kipindi mkalama inategemea kila kitu kutoka wilaya mama ya Iramba ilikuwa changamoto katika kupata baadhi ya huduma tofauti na sasa
Mkalama inajitegemea yenyewe katika kujiendesha kiutawala na hata huduma za kijamii kama ambavyo awali wananchi walikuwa wanazifuata Kiomboi.
“Kuna mafanikio mengi ambayo yamepatika na kutokana na kuwa na wilaya na Halmashauri yapo mambo mengi sana ambayo tulikuwa tunapata mkate mmoja tunagawana na wenzetu wa Iramba lakini sasa kila mmoja anapata wake, miaka 61 ya uhuru tuna mengi sana ya kujivunia”, Alisema Mkwega.
Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru yamefanyika Leo tar. 9/12/2022 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Iguguno huku yakiambatana na kauli mbiu isemayo " AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU ".
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.