Katika kuazimisha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara,Serikali ya Mkoa wa Singida na wanachi wake wanajivunia mafanikio makubwa ambayo yametokana na jitihada kubwa zilizofanywa na serikali ya awamu ya kwanza hadi ya sita .
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binirith Mahenge amesema hayo wakati akihutubia wananchi wa Mkoa wa Singida katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru Kimkoa yaliyofanyika katika , viwanja vya jumbe wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Aidha Dkt Mahenge amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 60 ya uhuru Mkoa wa Singida umeongeza tija katika sekta mbali mbali zikiwemo za uzalishaji mali na huduma za jamii,utawala bora,ulinzi na usalama,kilimo ,afya,elimu,viwanda na umeme.
‘’kwa kipindi cha miaka 60 ya uhuru tuanjivunia mkoa wetu kuwa na mafanikio mengi na makubwa ikiwemo kujitosheleza kwa chakula ,ongezeko la uzalishaji wa mazao ya biashara kama ufuta ,Alizeti,Korosho ,Dengu na vitunguu hii yote ni kutokana na kuongezeka kwa Teknolojia za kisasa kwenye sekta ya kilimo kama vile pembejeo, mbolea ,mbegu bora na hifadhi bora ya mazao’’alisema Dkt Mahenge Rc Singida.
Pamoja na hayo ametaja mafanikio katika uzalishaji wa mazao ya chakula na kusema umeongezeka kutoka tani 197,886 mwaka 1990 na kufikia tani 821,882 kwa mwaka 2020/2021 mara baada ya Mkoa kuainisha uzalishaji wa mazao ya chakula ya kipaumbele ambayo ni Mtama,uwele,viazi vitamu na Mihogo ,ambaapo uzalishaji wa mazao hayo yaliongezaka kutoka tani 194,878 kwa mwaka 2005/2006 hadi kufikia tani 395594 kwa mwaka 2020/2021 huku mazao ya biashara yakiongezeka kutoka tani 41,746 mwaka 2005/2006 hadi tani 230,793 mwaka 2020/2021 ambapo zao la alizeti pekee limeongezeka kutoka tani 28,917 kwa mwaka 2005/2006 hadi tani 222,800 kwa mwaka 2020/2021.
Hata hivyo hakusita kutaja mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya elimu kwa mwaka 1961 hapakuwa na madarasa ya shule za awali ambapo kwa 2021 kuna jumla ya madarasa ya awali 561 na kuongeza kuwa mkoa umefanikiwa kutoa elimu kwa walemavu ambapo kwa mwaka 1961 hapakuwa na shule ya walemavu ukilinganishwa na2021 shule zimeongezeka na kufikia 12.
Sanjari na hayo ametaja mafaniko katika sekta ya afya kuwa Mkoa una vituo vya kutolea huduma za afya 246 ,Hospitali 11 vituo vya afya 20 zahanati 211 huku akiongeza kuwa serikali inaendelea kujenga hospitali za wilaya 3 na kusema Mkoa umepokea fedha za tozo kiasi cha sh Billion .2.2 kwaajili ya vituo vya afya 9 kupitia mpango wa maendeleokwa ustawi wa taifa na mapambano ya UVIKO 19 huku Billion 1.9 kwaajili ya ujenzi wa majengo ya dharura katika hospitali za wilaya ,wagonjwa mahututi na nyumba za walimu.
Dkt Mahenge amewataka wananchi wa Mkoa wa Singida kutumia kikamilifu fursa za uwekezaji ili kuondokana na umasikini wa kipato na kuboresha hali ya Maisha ya wananchi kiuchumi na Kijamii
Kilele cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania bara Kimkoa yamefikia tamati leo ta 8/12/2021
Na kitaifa yanatarajiwa kufanyika hapo keshi 9/12/2021 jijini Dar-es-salaamu
Na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’MIAKA 60 YA UHURU,TANZANIA IMARA KAZI IENDELEE’’.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.