“RUDI MKALAMA, KUMENOGA!” Hiyo ndio kauli inayoweza kutumika hivi sasa baada ya Wilaya ya Mkalama kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa Halmashauri za Mkoa wa Singida kwenye maonesho ya 22 ya sikukuu ya wakulima na Wafugaji (NANENANE) yaliyohitimishwa leo hii na Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde.
Ushindi huo unatokana na Wilaya hiyo kujidhatiti kikamilifu katika sekta za Kilimo na Mifugo ambapo waliweza kuonesha kwa vitendo kwa kuotesha mimea mbalimbali inayolimwa Wilayani Mkalama kupitia mashamba yao yaliyopo hapa kwenye viwanja vya Nzuguni.
Mbali na mimea hiyo iliyostawi vizuri, Mkalama pia wameweza kuonesha ustadi wa kufuga samaki na kuku ambapo wataalam wa mifugo na uvuvi waliweza kuonesha namna bora kabisa ya kufuga kuku wa kienyeji na aina mbalimbali za samaki kupitia bwawa lililopo nyuma ya banda lao la Maonesho.
Katika hali inayoonesha kujipanga zaidi kwa Uongozi wa Wilaya ya Mkalama katika maonesho yajayo, Wilaya hiyo imeshatengeneza mabanda ya kufugia Ng’ombe na Mbuzi hivyo kwa wageni watakaotembelea banda hilo kwenye maonesho ya mwaka 2019 watapata fursa ya kujifunza namna bora ya kufuga ng’ombe na mbuzi.
Mkalama Guntooooooo!
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.