• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Madaktari bingwa watoa huduma Mkalama

Imewekwa kwenye: March 23rd, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe: Rehema Nchimbi jana alifanya ziara Wilayani Mkalama ambapo alitembelea na kukagua miradi mbalimbali na kuzindua zoezi la madaktari bingwa linaloendelea katika hospitali ya Iambi.

Mara baada ya kufika katika hospitali ya Iambi, Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki alimsomea Mhe: Nchimbi  taarifa fupi ya zoezi hilo na jinsi lilivyofanyika katika Mkoa wa Singida ambapo taarifa hiyo ilieleza namna zoezi hilo lilivyofanyika kwa mafanikio huku likitarajiwa kuhitimishwa katika Wilaya ya Mkalama.

“Mpaka sasa jumla ya watu 675 wameonwa na madaktari bingwa na 71 kati yao wamefanyiwa upasuaji” Alisema Mwombeki.

Akizungumza mara baada ya kusomewa taarifa, Mhe: Nchimbi alimpongeza Mganga Mkuu wa Mkoa na timu yake kwa kufanikisha kufanyika kwa zoezi hilo ambapo alizitaka Halmashauri zote Mkoani Singida kuangalia namna ya kupata shilingi Milioni 18 kila Mwaka kwa ajili ya huduma za madaktari bingwa.

“Halmashauri zisisubiri kufuatwa na Mkoa kwa ajili ya zoezi hili bali ziandae ratiba na kuziwasilisha Mkoani ili zoezi hili liwe endelevu” Alisema Mhe: Nchimbi.

Aliongeza kuwa utengenezwe mfuko maalum kwa ajili ya zoezi hilo ili pesa inayopatikana katika mazoezi ya madaktari bingwa iwekwe humo kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linakuwa endelevu.

Kabla ya kuzindua zoezi la Madaktari bingwa, Mhe: Nchimbi alitembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii kilichopo katika kata ya Gumanga ambapo aliiagiza halmashauri ya Wilaya ya Mkalama iandae taarifa ya miaka mitano ya chuo hicho.

“Halmashauri ni lazima ikichukue chuo hiki na ihakikishe kinapata wanafunzi wa kutosha na viongozi wa Chuo ni lazima wabadilike na kutoa mapendekezo mazuri ya uendelezaji wa Chuo hiki”. Alisema Mhe: Nchimbi.

Alisema kuwa Mkoa na Halmashauri watumie chuo hicho kama sehemu ya mafunzo kwa watendaji wa kada zote na kisigeuzwe shule ya  kidato cha tano kama ilivyopendekezwa  bali halmashauri itafute mahali pengine na kuhakikisha inakuwa na shule ya ngazi ya kidato cha tano mwaka huu.

Alihitimisha kwa kuziagiza halmashauri zote Mkoani Singida kununua camera na vifaa vingine vya kisasa vitakavyowawezesha maafisa habari kufanya kazi zao kwa ufanisi badala ya kuwaacha wataalam hao kuendelea kutumia vyombo binafsi.

“Haiwezekani hawa wataalam wa serikali kuendelea kutumia vyombo binafsi, vyombo vina “filosofia” zao , tuwe na matukio yetu tuyaandae na kuyatangaza kwa sababu moja ya vitu vikubwa vinavyochagiza maendeleo ni kupata taarifa au habari” Alimalizia Mhe” Nchimbi.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.