Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Daktari Rehema Nchimbi jioni hii ametembelea banda la bidhaa mbalimbali na maeneo ya maonesho ya Nane nane ya Wilaya ya Mkalama ambapo ameupongeza uongozi wa Wilaya hiyo kwa kuboresha banda na maeneo yote yenye bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wakulima na wafugaji wa Wilaya ya Mkalama.
Katika ziara hiyo Mhe. Nchimbi ameuagiza uongozi wa Wilaya ya Mkalama kuhakikisha maeneo hayo yanaendelea kuzalisha hata mara baada ya maonesho ya Nanenane kumalizika ili hatimaye Mkalama iwe ni moja ya wilaya inayozalisha bidhaa za kutosha ndani ya Mkoa wa Dodoma.
“Pia sehemu ya eneo lililobaki wapeni wakulima wa Mkalama ili waweze kuzalisha mazao yao misimu yote kisha mnaweza kuweka utaratibu wa kugawana asilimia kadhaa ya mapato yanayopatikana kutokana na mavuno ya mazao hayo’’ Ameongeza Mhe. Nchimbi.
Mhe. Nchimbi amebainisha kuwa kufanya hivyo kutaifanya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama iwe imetekeleza sera ya kupeleka vijijini asilimia 10 za wanawake na vijana kwa vitendo ambapo itakuwa ina kiashiria kinachoonekana cha utekelezaji wa sera hiyo.
‘’Pia niwakumbushe viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kuwa wakulima wameshatimiza wajibu wao kwa kulima mazao na kuyasindika katika bidhaa tofauti hivyo ni wajibu wenu kuhakikisha mnawatafutia soko la bidhaa hivyo na kufanya hivyo sio tu kutawanufaisha wakulima bali kutasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri yenu’’ Amesisitiza Mhe. Nchimbi.
Katika kuwaunga mkono wajasiriamali wa bidhaa za kilimo wilayani Mkalama, Mhe. Nchimbi alinunua bidhaa zenye thamani ya shilingi elfu 58 aliowakuta katika banda hilo la maonesho.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.