Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali ametaka watumishi wapya waliopangiwa na Serikali Wilayani Mkalama kufanya kazi kwa bidii na kujiamini ili kumwakilisha vyema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kuwaamini na kuwapa dhamana ya kuwatumikia wananchi.
Ameyasema hayo (Julai 29 2023) wakati akiongea na watumishi hao katika hafla maalumu ya kuwakaribisha watumishi wapya wa kada mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa Sheketela Wilayani Mkalama.
Mhe. Machali aliwataka watumishi hao wapya kuwa mfano kwa wengine na kuwa waaminifu katika kazi yao ya kuwatumikia wananchi, pia kuwataka kujiepusha na vitendo viovu vinavyoharibu taswira yao pamoja na Taasisi wazozitumikia.
‘’Nendeni mkafanye kazi ,serikali inawategemea na kuwaamini nendeni mkailipe Imani serikali yenu na kuilipa kwenu ni ninyi kufanya kazi kwa bidi alisisiza’’ Mhe. Machali
Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya Katibu Tawala Wilaya ya Mkalama Mhe. Peter Masindi aliwapongeza watumishi wapya kupata nafasi ya kutumikia Wilaya ya Mkalama ambapo aliwasihi kuzitendea haki nafasi hizo kwakufanya kazi zenye kiwango na ubora .
‘’Leo hii mmepata nafasi mkiwa na umri mzuri kabisa na hapa mmeanzisha safari ya kuelekea kustaafu , mnatakiwa kuonyesha mlichonacho na kutumia muda wenu vizuri kwakufanya mambo makubwa na yenye ubora’’. Aliongeza Mhe. Masindi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Asia Messos amesema kuwa Halmashauri ilipata kibali cha kuajiri watumishi 145 lakini hadi kufikia leo watumishi 139 wameripoti na wanaendelea na majukumu yao kama kawaida huku akiwataka kufanya kazi kwa bidii na kutekeleza majukumu waliyopangiwa kutokana na kuwa kuna watumishi wengi wapo mtaani walitamani nafasi hizo lakini wakapatiwa wao.
Hafla hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Idara na vitengo, Wakuu wa Taasisi za Kifedha ,Benki ya NMB ,NBC,CRDB pamoja na viongozi wa vyama vya wafanyakazi ambavyo ni TALGWU,TUKUTA na CWT ambao wote kwapamoja waliwasilisha mada kuhusu haki na wajibu wa mtumishi pamoja na nidhamu ya fedha .
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.