Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Moses Machali ameendelea na ziara ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero kwa wananchi wa vijiji vya Senene na Lukomo kata ya Iguguno wilayani Mkalama.
Akizungumza kwa nyakati tofauti Aprili 23,2024 katika vijiji hivyo, Mhe. Moses Machali amepiga marufu mchezo wa Pool Table, wazazi wawapeleke watoto kuchoma chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi pamoja na kuachana na michepuko.
“Vijana waende wakafanye kazi, marufuku michezo ya Pool Table asubuhi, Kaaeni na vijana wenu, wafundisheni maadili, wasiwe na haraka ya kufanikiwa maisha kwa njia zisizo halali” Mhe.Moses Machali
“Zungumzeni na watoto wenu, wekezeni katika maadili, Jamii imeharibika. Chunguzeni watoto wenu wanapotoka shuleni, Tuwalinde watoto wetu, na tusiozeshe mabinti wakiwa bado wadogo” Mhe.Moses Machali
Akizungumzia kuhusu chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi iliyoanza kutolewa kiwilaya Aprili 23,2024, Mhe.Moses Machali awewataka wazazi kuhakikisha watoto wao wakike wanachanja ili kuepukana na ugonjwa huo.
“Saratani ya mlango wa kizazi ni hatari, ni tatizo kubwa linalowakabili kina mama waambieni watoto wachanje,ni chanjo safi na salama. Kina Baba, Kina Mama acheni michepuko UKIMWI upo. Mhe.Machali
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.