Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe . Moses Machali amepiga marufuku uchezaji wa mpira wa meza maarufu kama "Pool table" wakati wa muda wa kazi.
Mhe. Machali ametoa marufuku hiyo leo Februari 20, 2023 wakati wa kikao na Viongozi wa ngazi mbalimbali Wilayani Mkalama ambapo amemuelekeza Mkuu wa Polisi wilayani hapo kuhakikisha wanafuatilia suala hilo ambalo linazorotesha uchumi wa wilaya na Taifa kwa ujumla
‘’ Kaimu Mkuu wa Polisi ninakuagiza leo hakikisha unafanya oparesheni kwa yeyote wanaohusika kamata Sukuma ndani na tuwapeleke Mahakamani tuwatie adabu ’’ Alisisitiza Mhe. Machali
Aidha Mhe. Machali ameagiza mchezo huo ufunguliwe kuanzia saa kumi joni Pamoja na baa zote Wilayani Mkalama ili kupisha muda wa kazi kwa vijana na watu wengine kwa maslahi mapana ya Wilaya hiyo.
Aidha amesema Ofisi yake haitafumbia macho suala hilo ambapo ameongeza kuwa atawachukulia hatua kali za kisheria wamiliki wa bar wote watakao kiuka agizo lake.
‘’Haiwezakani vijana na watu wengine wazima wanaamka asubuhi wanaenda kucheza "pool table" unakuta kijana analiwa pesa zote mwisho wa siku anaanza kukuibia na wewe mzazi na hatimaye tunazalisha vibaka’’ Aliongeza Mhe. Machali
Sheria ya Vileo ya mwaka 1967 imeelekeza muda mahususi wa Vilabu vya pombe ambapo lengo la Sheria hiyo ni kutoa fursa kwa wananchi kutenga muda wa kufanya shughuli nyingine za maendeleo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.