Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali leo amefanya ziara ya kikazi katika kijiji cha Asanja kata ya Ilunda na kijiji cha Mwanga kata ya Mwanga wilayani Mkalama kusikiliza na kutatua kero zinazowakabili wananachi wa vijiji hivyo.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Asanja na Mwanga Machi 18,2024, Mhe. Machali amepiga marufuku kukodishwa kwa mashamba ya shule, kuuzwa kwa maeneo ya serikali,wafanyabiashara kubeba lumbesa ,wakulima kuuza mazao yao shambani , pamoja na kuwataka wananachi kudumisha amani na upendo
“Marufuku kukodisha mashamba ya shule. mashamba ya shule yatumike kwa ajili ya kuzalisha chakula kwa wanafunzi. Nisisikie Mtu anakodisha shamba la shule.Msiuze Ardhi ya serikali bila sababu, msipokuwa makini mtakuja kufanywa manamba hapa” Mhe. Moses Machali
“Wakulima Marufuku kuuza mazao shambani, Nisisikie suala la wafugaji kupeleka mifugo yao katika mashamba ya watu. Tabia ya kuoneana si nzuri na pia tudumishe amani na upendo” Mhe. Moses Machali
Awali akijibu maswali kuhusu sualala maji safi na huduma ya umeme katika vijiji vya Asanja na Mwanga, Mhe Machali amewaambia wananchi kuwa serikali tayari imeweka mpango wa kupeleka huduma ya maji safi na salama pamoja na huduma ya umeme katika vitingoji ambavyo havijafikiwa na umeme.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.