Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba Leo ameupokea Mwenge wa uhuru kutoka Mkoa wa Tabora ambapo Mwenge huo utakua Mkoani Singida kwa siku Saba katika Halmashauri zote za Mkoa wa Singida.
Aidha amesema Mwenge ukiwa Mkoani Singida utakimbizwa Kwa kilomita 981.7 na utapitia miradi ya Maendeleo 35 inayohusu elimu, Afya ,utalawa Bora, Maji , barabara uwezeshwaji vijana kiuchumi pamoja na programu 42 za sensa, rushwa , Maralia mapambano dhidi ya madawa ya kulevya,VVU na UKIMWI pamoja na masuala ya Lishe
Pamoja na hayo Mhe. Serukamba alisema kuwa jumla ya miradi 18 itazinduliwa na Mwenge wa uhuru, miradi 11 itawekwa jiwe la Msingi pamoja na kutembelea na kukagua miradi 6 , miradi yote itakayotembelewa na kupitiwa na Mwenge wa uhuru Mwaka 2022 itakua na thamani ya Tsh. 8,280,426,339.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.