Afisa Elimu ya Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mwalimu Jusline Bandiko amewataka Maafisa Elimu Kata Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kutumia vizuri nafasi zao katika kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu wilayani Mkalama.
Wito huo ameutoa Julai 15,2024 wakati wa mafunzo ya Usimamizi Saidizi yanayotolewa na serikali kupitia mradi wa Shule Bora yanayofanyika katika shule ya sekondari Mkalama One iliyopo kata ya Nduguti wilayani Mkalama
“Kwa mafunzo haya ya leo binafsi naona ni ufunguo mzuri ambao utatufanya tufanye kazi za matokeo. Wito wangu kwenu tujipange kufanya kilicho sahihi, si kwa ajili yetu, kwa ajili ya wale tunao wahudumia” Mwalimu Bandiko
Akinzungumza kwa niaba ya Maafisa Elimu Kata waliodhuria mafunzo hayo, Mwalimu Chitara Haruni Afisa Elimu Kata Nduguti amesema mafunzo hayo yatasadia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha usimamizi katika maeneo ya kitaaluma na kupelekea kuongezeka kwa ufaulu kwa wanafunzi.
“Tunawashukuru Shule Bora kwa mafunzo haya, kupitia mafunzo tuliopata hapa yatasaidia katika usimamizi wetu wa kitaaluma na hivyo kupelekea kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi ndani ya wilaya yetu” Mwalimu Chitara Haruni
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.