Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Mhe. James Mkwega amewataka Madiwani kushirikiana pamoja kuijenga Kata ya Nduguti kwani ndio Makao Makuu ya Wilaya.
Ameyasema hayo mapema leo (Agosti 1,2023) katika Baraza la Madiwani la Robo ya Nne kwakipindi cha April- Juni 2023 ambalo lilihusisha kamati mbalimbali kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Serikali kwa kipindi cha miezi Mitatu.
Mhe. Mkwega alitumia nafasi hiyo kuwataka madiwani kwa umoja wao kuungana pamoja kuisemea Kata ya Nduguti iweze kupata miradi mingi ya maendeleo kwani ndio Taswira na kioo cha Wilaya.
‘’kwa kuwa Nduguti bado ni Kijiji tunahitaji kwanza Taasisi zijae hapa mjini ili watu wakija waone kuna Shule ya Kidato cha Tano na Sita, Shule Maalum na Soko la Kimkakati lipo mjini hapa, Kuwa na Makao Makuu ya Wilaya ni neema, tusiipime Nduguti na Kata nyingine kwa kila jambo huu mji tutaudhoofisha’’ Alisistiza Mhe.Mkwega
Pamoja na hayo aliwataka Maafisa Tarafa kuisaidia Halmashauri kuzunguka Shuleni kuhamasisha suala la Lishe pia kuhakikisha Kata zinakuwa na ratiba ya kufanya mikutano kwa wakati ili jamii ipata taarifa zote zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Shupavu wa awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Hussein Mwatawala , Kaimu Afisa Tawala Mkoa wa Singida, alitumia nafasi hiyo kuupongeza Uongozi wa Wilaya ya Mkalama kushika nafasi ya pili katika ukamilishaji wa Miradi ya BOOST pamoja na kushika nafasi ya kwanza katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa asilimia 109 hivyo kuwataka kuendelea na Ushirikiano waliona katika kuchochea Maendeleo ya Wilaya.
Akimwakilisha Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Afisa Tarafa ya Kinyangiri, Bw. Isack Kimaro amesisitiza wananfunzi wote wa shule za Msingi na Sekondari kupata chakula shuleni, hivyo waheshimiwa madiwani wanawajibu wa kuhamasisha jamii kuchangia chakula.
Mwenyekiti wa CCM wilaya, Bw. Lameck Itungi Amepongeza Uongozi wa wilaya kwa kutekeleza miradi ya maendelea kwa weledi na kuwataka Viongozi kukemea upotoshaji unaoendelea kwa baadhi ya watu kuhusu uwekezaji wa Bandari.
MKALAMA DISTRICT COUNCIL
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.