MADIWANI MKALAMA WAOMBA SHERIA YA WANYAMA PORI IBORESHWE
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida wameiomba serikali kuifanyia mabadiliko sheria ya malipo ya fidia kwa wananchi ambao mazao yao yanaharibiwa naTembo mashambani kwani kiwango kinachotolewa kwa waathirika ni kwasa ni kidogo ukilinganisha na athari zinazozababishwa na Tembo hao.
Ombi hilo limetolewa na Diwania wa kata ya Mwangeza,Bosco Samweli, wakati wa kikao cha Baraza la wazi la Madiwani cha cha robo ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2023/24 kilichofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Novemba 29/2023.
Diwani Bosco Samweli alisema maeneo mbalimbali katika Wilaya ya Mkalama wananchi wamekuwa wakikubwa na uvamizi wa tembo kwenye nyumba zao na uharibifu wa mazao mashambani lakini kiwango cha Sh.100, 000 kinachotolewa kwa waathiriwa wa mashamba na Sh.1, 000,000 kinachotolewa kama kifuta jasho kwa wanaopoteza maisha ni kidogo sana hivyo kuna haja ya kubadili sheria ili kiwango cha malipo ya fidia na kifuta jasho kiongezeke.
Akijibu hoja hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama,Abdalla Njelu, amesema ni kweli wilaya hiyo wananchi wanapata sana changamoto ya tembo na kwamba suala la kutaka kiwango cha malipo na fidia na kifuta jasho kiongezwe wataliwasilisha katika ngazi husika
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.