Katibu Tawala mkoa wa Singida Dkt. Fatuma Mganga amewata wazazi mkoani Singida kutimiza wajibu wao kila mmoja katika familia ili kuwa na jamii bora kwa maendeleo bora ya taifa letu. Kauli hiyo ameitoa Mei 15/2024 wakati wa Kongamano la siku ya Familia Duniani lililofanyika kimkoa katika kata ya Ibaga wilayani Mkalama na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, dini pamoja na wananchi.
“Kila mmoja atimize wajibu wake, tusaidiane, tushirikiane tuweze kulea familia vizuri, lakini pia tusilee watoto wetu kama mayai, tufuatilie mienendo ya watoto wetu,suala la kutengeneza familia bora si suala la serikali, ni suala la la kila familia. Wazazi tutimize wajibu wetu tusiwachekee watoto wetu” Dkt. Fatuma Mganga
“Baba ni kichwa familia, Kina Baba mnalojukumu kubwa la kusimamisha familia. Kina baba chukueni nafasi yenu katika familia tuweze kuongoza familia mahali inapostahili” Dkt. Fatuma Mganga
Awali akiwasilisha hoja kuhusu chanzo cha familia nyingi kuvunjika, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe.Moses Machali amesema kukosekana kwa uwazi baina ya wana ndoa pia kunapelekea ndoa nyingi kuwa na migogoro. "Ushirikishwaji katika familia ni muhimu. Pale panapokosekana ushirikishwaji katika familia kunaleta shida.Tubadili tabia zetu, tufanye kazi ,kama ni kulima , Baba lima sana, kama ni Mama, fanya kazi, kazi ya kutunza familia ni jukumu letu sote" DC Machali
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.