Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewataka Watendaji wa Vijiji, Kata, Maafisa Tarafa, pamoja na watumishi Afya kuwaelimisha wananchi kuzingatia usafi sambamba na kuhakikisha kila kaya ina jenga choo katika kupambana na tishio la mlipuko wa ugon amewataka Watendaji wa Vijiji, Kata, Maafisa Tarafa, pamoja na watumishi Afya kuwaelimisha wananchi kuzingatia usafi sambamba na kuhakikisha kila kaya ina jenga choo katika kupambana na tishio la mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu wilayani Mkalama.
ametoa agizo hii Leo tarehe 12/01/2024 wakati wa mkutano wa dharula na wakuu wa idara, watendaji wa vijiji, kata , maafisa tarafa na watumishi wa afya wa kujadili tahadhali ya mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu uliofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama
“Watendaji wa Vijiji,Kata, Maafisa Tarafa, watu wa Afya shirikianeni kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo, ambao hawatachimba choo wapigwe faini. Sitaki kusikia mtu hana choo.Natoa miezi 3 shule zote zinakuwa na vyoo, changisheni michango wananchi kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule zetu” DC Machali
“Waelimisheni Mama lishe, Baba Lishe, wachoma mahindi wazingatie usafi, wananchi watumie maji ya kuchemsha au yaliyotibiwa kwa dawa na vilabu vyote vya pombe ambavyo havina vyoo vifungwe mara moja” DC Moses Machali.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa wilaya ya Mkalama Bi Asia Messos amewataka walimu kuhakikisha kila siku wanawaelimisha wanafunzi kuhusu ugonjwa wa kipindupindu kwa kuzingatia matumizi ya maji safi na salama, kuweka vyoo vya shule safi muda wote katika kuhakikisha wanadhibiti ugonjwa wa Kipindupindu
Awali akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya ugonjwa wa Kipindupindu wilayani Mkalama, Afisa Afya wilaya , Dorice Damian amesema hadi kufikia Novemba 06,2023 idadi ya watu walioripotiwa kuwa na Kipindupindu walikuwa ni 9 na hakuna kifo chochote kilichoripotiwa kinachotokana na ugonjwa huo huku wagonjwa hao tayari wamesharuhusiwa kurudi majumbani kwao kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.