Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu Godfrey Mnzava ameipongeza serikali kwa kuanzisha mfumo wa manunuzi wa NeST kwa ajili ya kuweka uwazi wa manunuzi mbalimbali serikalini.
Kauli hiyo ameitoa Julai 10,2024 wakati wa kuweka jiwe la Msingi kwenye mradi wa barabara ya Gengerankuru Moma iliyojengwa kwa kiwango cha lami kutoka serikali kuu.
“Serikali inafanya mambo makubwa, imeleta mfumo mzuri wa manunuzi ya Umma lengo likiwa ni kuweka uwazi na kuondoa hisia kuwa kuna upendeleo, kuondoa mianya ya Rushwa, tuzingatie matumizi ya mfumo huu kwa maendeleo ya taifa letu” Mnzava
Awali akiwasilisha taarifa kuhusu ujenzi wa barabara hiyo kwa niaba ya Meneja wa TARURA wilaya ya Mkalama, Mhandisi Paschal Mafuru amesema mradi huo umejengwa kwa kuzingatia mfumo wa manunuzi ya serikali NeST na umegharimu kiasi cha shilingi 502,474,000.00
“Mradi huu umegharimu shilingi 502,474,000.00 fedha kutoka serikali kuu, mradi huu umerahisisha huduma kwa wananchi wa Mkalama wanaofika ofisi ya Mkuu wa wilaya kupata huduma na pia umetoa ajira za muda mfupi kwa watu 120, wanawake 12 na wanaume 108” Mhandisi Mafuru
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 wilayani Mkalama zimezindua mradi mmoja na kuweka jiwe la Msingi katika miradi miwili ambapo miradi yote hii imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 2.1
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.