Wakulima wameshauri kulima zao la Pamba kwa kuzingatia Kilimo cha kisasa na kufuata kanuni Bora za kilimo ili kuongeza thamani katika zao hilo na kujikwamua na hali duni ya maisha.
Hayo yamesemwa na Bw. Juma Salum Mkaguzi wa zao la Pamba kwa Wilaya ya Mkalama na Iramba wakati akitoa mafunzo elekezi ya namna ya kulima zao la Pamba kwa tija katika Vijiji vya Lugongo,Nyahaa na Mpambala Kata ya Ibaga wilayani Mkalama Mkoani Singida.
Bw.Salum amesema kuwa zao la Pamba litamkwamua Mkulima katika hali duni ya maisha endapo watazingitia kanuni za kilimo ikiwa ni pamoja na kuandaa shamba mapema,kuweka mbolea pamoja na kupanda kwa wakati.
"Tumekuja kuhamasisha wananchi kulima zao la Pamba lengo likiwa ni kuongeza Tija kwenye zao hili kwa kuzingatia kipindi sahihi cha upandaji wa zao la Pamba ambapo tunashauri kuanzia tar 15 /11 hadi tar 15/12 Mkulima awe amepanda mbegu kwa kuzingatia vipimo sahihi pia kupalilia kwa wakati pamoja na kuvuna kwa wakati ili kuongeza tija katika uzalishaji wa pamba " aliongeza Bw.Juma Salum Mkaguzi wa zao la Pamba.
Aidha ameongeza kuwa ili kuongeza uzalishaji wa zao la Pamba wilayani Mkalama serikali kwakushirikiana na Bodi ya Pamba Tanzania itatoa mbegu kwa wakulima kwa Mkopo pamoja na kutoa elimu kwa maafisa Ugani na wakulima ili wawe mabalozi kwa wengine.
Baadhi ya wakulima wa Vijiji vya Lugongo Nyahaa na Mpambala wameishukuru serikali kupitia bodi ya pamba kutoa elimu ya uhamasishaji wa kilimo cha zao la pamba ambapo wamesema kuwa watazingitia kanuni walizofundishwa huku wakiiomba serikali kuhakikisha wanapeleka pembejeo mapema pamoja na kuwa na soko la uhakika.
Frank Lupogo kutoka shirika la Biosustain wanaojihusisha na ununuaji wa pamba amewahakikishia wakulima kuwa watanunua Pamba kutokana na bei elekezi itakayopangwa hivyo kuwataka kuondoa hofu kwani uhakika wa soko upo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.