Jamii imetakiwa kusimama na kupinga ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa Watoto ili kuwa na taifa imara na lenye nguvu kwa kizazi kijacho.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Mkoa wa Singida Bi Doroth Mwaluko katika kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsi yaliyofanyika Kimkoa katika ukumbi wa Sheketela uliopo wilaya Mkalama Mkoani Singida.
Aidha Bi. Mwaluko amesema kuwa kila mtu ana wajibu wa kuripoti na kupinga ukatili wa kijinsia na kutetea haki za Watoto kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vile mavazi,malazi, chakula pamoja na haki ya kupata elimu kwa wote kwakuzingatia usawa wa kijinsia.
Awali akisoma taarifa kwa mgeni rasmi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa amesema kuwa kesi zinazotokana na ukatili wa kijinsia zimepungua kutoka 1012 kwa mwaka 2019 /2020 na kufikia 924 kwa kipindi cha mwaka 2020/2021 .
Ameongeza kwa kusema kuwa sababu zinazopelekea kupungua kwa matukio ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa Watoto kuwa ni elimu inayoendelea kutolewa kwa jamii inayosimamiwa na kitengo cha dawati la jinsia kwa ngazi ya wilaya ,kata na vijiji .
Pamoja na hayo ACP Mutabihirwa ameendelea kukemea tabia za baadhi ya wazazi wanaopewa pesa na mali ili kufuta kesi za Watoto wanaofanyiwa ukatili wa kijinsi kama vile kubakwa ,kulaitiwa nakukatishwa masomo kutokana na mimba za utotoni zinapofika mahakamani huku akiwata wazazi hao kutumia siku hii adhimu kupinga na kukemea vikali matukio ya ukatili wa kijinsia ili kuweza kumaliza kabisa tatizo hilo.
Akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia kizigo amesema kuwa siku hii ya kupinga ukatili wa kijinsia uzingatie jinsia zote usiegemee upande mmoja .
‘’Ili tuwe na taifa imara ni lazima tuwe na usawa ,wakati dunian nzima tunaenda kumkomboa mtoto wa kike tumemsahau mtoto wa kiume, tusije tukatengeneza maadhimisho mengine tena ya kumkomboa mtoto wa kiume maana wamesahaulika, Watoto wakiume wamekuwa wakifanyiwa mambo ya kikatili lakini jamii imenyamaza kimya’’.Ameongeza mhe.Sophia kizigo Dc Mkalama.
Maadhimisho ya siku ya ukatili huazimishwa Disemba 10 ya kila mwana na
Kaulimbiu ya Mwaka huu ni ‘’EWE MWANANCHI KOMESHA UKATILI WA KIJINSIA SASA”
‘’SINGIDA BILA UKATILI WA KIJINSIA INAWEZEKANA’’.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.