Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Peter Serukamba ametoa agizo kwa maafisa ugani na maafisa elimu Kata Wilayani Mkalama kukaa katika maeneo yao ya kazi ili kuongeza ufanisi katika kazi zao.
Ametoa agizo hilo Januari 08,2023 wakati wa kikao kazi na Madiwani, Maafisa Ugani, watendaji wa kata, vijiji pamoja na wakuu wa idara na Vitengo kilichofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
" Maafisa ugani, maafisa elimu wote waishi katika maeneo yao ya kazi, tuandae vipimo vya kupima utendaji kazi wa maafisa ugani, kila mwezi ametembelea wakulima wangapi? kila mwezi ameandikisha wakulima wangapi? kuwaelimisha wakulima jinsi ya kulima kisayansi" Mhe. Serukamba
Mhe. Serukamba amewataka watendaji kuongeza uzalishajikwa kufuata taratibu za kilimo,kilimoambapo amewaomba Madiwani kutumia vikao vyao kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya mbolea ili kuongeza uzalishaji Wilayani hapa ambapo pia ambapo alimuagiza Afisa kilimo wilaya kufanya vikao na maafisa Kilimo wa Kata pamoja na Maafisa ugani kilamara ili kuongeza ufanisi wao kazini.
Katika hatua nyingine Mhe. Serukamba ametoa wito kwa Maafisa elimu wilaya kusimamia zoezi ka uandikishaji wanafunzi sambamba na kupunguza tatizo la utoro Shuleni.
Naye Afisa Kilimo Wilaya ya Mkalama Bw. Selemani Msunga amesema hali ya matumizi ya mbolea kwa wilaya ya Mkalama ni nzuri kiasi kwamba matumizi ya mbolea kwa wakulima yamevuka lengo lillokuwa limewekwa ambapo amesema kama Wilaya ilikusudia kutumia tani 1500 lakini kwa sasa matumizi yamefikia zaidi ya tani 2000
Akiongea kwa naiba ya Madiwani Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhe. James Mkwega amesema kama madiwani watahakikisha wanawahamasisha wananchi kulima kisasa na kuongeza uzalishaji kwakutumia mbolea pamoja na mbegu bora ambapo pia aliwataka watendaji, Maafisa ugani pamoja na Maafisa Tarafa kutekeleza majukumu yao vizuri kwakuwatembelea wananchi na kuacha kukaa maofisini.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.