Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mhe: Jackson Masaka amewataka wazazi na walezi wote Wilayani hapa kuhakikisha wanapeleka shuleni watoto wote waliochanguliwa kujiunga na idato cha kwanza na wale ambao bado hawajaandikishwa kujiunga na elimu ya awali na msingi waandikishwe kwa wakati kabla shule hazijafungua.
Mhe: Masaka ameyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya jeshi la Akiba maarufu kama Mgambo yaliyoenda sambamba na sherehe za maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanganyika katika uwanja wa mpira wa Miguu wa Iguguno uliopo katika kata hiyo ambapo alisisitiza kuwa serikali haitasita kuchukua hatua kwa mzazi au mlezi atakayepuuzia agizo hilo kwa sababu dhamira ya dhati ya serikali iliyopo madarakani ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata Elimu na ndio maana imefuta malipo ya ada kutoka ngazi ya awali mpaka kidato cha nne.
“Ningependa kuchukua fursa hii kuwapongeza sana vijana kwa ujasiri na ukomavu waliouonesha katika kipindi chote cha mafunzo na ninawahakikishia serikali itakuwa bega kwa bega na nyinyi pindi zitakapokuwa zikitokea nafasi zinazohitaji ujuzi na mafunzo mliyoyapata” Alisisitiza Masaka.
Katika hatua nyingine, Mhe: Masaka aliwahimiza wananchi kuhifadhi chakula walichopata wakati wa mavuno ya msimu uliopita wa kilimo kwa sababu kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, Mikoa ya Dodoma na Singida itakuwa na mvua ya wastani kwa msimu wa mwaka 2016/2017 hivyo kuna hatari ya kukumbana na ukame kama wananchi hawatotunza chakula cha akiba.
“Tulime mazao yatakayohimili ukame kama vile mtama,uwele, viazi na mhogo lakini pia ili tujihakikishie kuwa na pesa ya kununua chakula kutoka maeneo mengine tuweke vipaumbele kwenye mazao ya biashara zaidi” Alimalizia Masaka.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.