Naibu Waziri wa Afya, Mendeleo ya jamii, jinsia na watoto, Mhe: Hamisi Kingwangala amefanya ziara Wilayani hapa wikiendi hii ambapo mbali na kutembelea na kukagua kazi mbalimbali zinazofanywa na Idara ya afya, ametoa maagizo Katika ziara hiyo, Kigwangala alianza kwa kutembelea Zahanati ya Nduguti ambapo alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mkalama kuhakikisha anamaliza ujenzi wa Jengo la Kituo cha Afya cha Wilaya ndani ya Miezi sita.
“Kama mtaendelea kusubiri pesa za bajeti ili mkamilishe jengo hili mtakuwa mnajichelewesha wenyewe kwa sababu kwa hatua lililofikia mna uwezo wa kulimalizia kwa kutumia vyanzo vya ndani” Aliongeza Kigwangala.
Katika hatua nyingine, Mhe: Kigwangala alimsifu mhudumu wa Zahanati hiyo, Josephine Mwakanyaga ambaye ndiye aliyekuwa akimpa maelezo mbalimbali yanayohusu zahanati hiyo kwa uwezo mkubwa alionao katika uchambuzi wa dawa na vifaa tiba.
“Huyu ni mhudumu mwenye uwezo mkubwa sana na anayejua kitu anachofanya” Alisema Kigwangala.
Ziara ya Mhe: Kigwangala ilihitimishwa katika Zahanati ya Iguguno ambapo alimsifu Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe: Allan Kiula na timu yote ya Halmashauri ya Wilaya kwa hatua waliyolifikisha jengo jipya linalotarajiwa kuwa kituo cha afya katika eneo hilo.
“Nawapongeza sana na ninawaahidi kuwaunga mkono kwa kuhakikisha taratibu za usajili wa kituo hiki zinafanyika haraka sana ili lianze kutumika mara moja mara baada ya kukamilika” Alimalizia Kigwangala.
Aidha katika kuunga mkono jitihada za Mhe: Kiula, Kigwangala aliahidi kuchangia shilingi milioni moja ili kukamilisha ujenzi wa Jengo hilo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.