• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Kila kata ifanye kampeni hii- DC

Imewekwa kwenye: November 23rd, 2018

“Ninaagiza kampeni hii ifanyike katika kata nyingine zote 16 zilizobakia za Wilaya yaMkalama”

Hilo ni agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mhandisi Jackson Masaka wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upimaji wa hiyari wa  virusi vya ukimwi iliyopewa jina la “Furaha Yangu” uliofanyika leo katika kijiji cha Nkalakala ambapo zaidi ya watu 250 walijitokeza kupima.

Katika hotuba yake Mhe. Masaka alimshukuru Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kwa kuzindua kampeni hiyo kitaifa yenye lengo la kuhamasisha wananchi hasa wanaume kujitokeza kwa wingi katika vituo vya afya kupima kwa hiyari virusi vya ukimwi.

“Kwa Wilaya ya Mkalama suala la kupima afya sio jipya kwetu kwa sababu nimeshuhudia watu wengi sana wakijitokeza kupima afya zao kipindi cha mkesha wa Mwenge na sherehe nyingine huku vipimo mbalimbali vikifanyika ikiwemo shinikizo la damu, Malaria na HIV/VVU” aliongeza Mhe. Masaka.

Mhe. Masaka aliwasisitiza wananchi wote wa Mkalama kuchukua tahadhari kwa kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya Ukimwi ili kuweza kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo ambayo kwa mkoa wa Singida imeonekana kukua kwa asilimia 0.3 kutoka asilimia 3.3 ya mwaka 2011/2012 hadi asilimia 3.6 ya mwaka 2016/2017.

“Lakini pia ninaomba wananchi msipuuze pindi mnapobanwa na vikohozi visivyoisha kwa sababu huenda ikawa ni dalili ya ugonjwa wa Kifua kikuu kwa hiyo usijikaushe ewe dada na kaka nendeni mkapime na bahati nzuri Wilaya yetu imepata wahisani wa kusaidia mapambano dhidi ya virusi vya Ukimwi na TB  na kampeni hizi ni msaada mkubwa kwa afya zetu” Aliongeza Mhe. Masaka.

Mhe. Masaka alihitimisha hotuba yake kwa kuwahimiza wananchi wote kuwashawishi vijana na watoto wao wasome kwa bidii masomo ya sayansi ili waweze kupata nafasi za kusomea uuguzi, ukunga, maabara, udaktari na kozi nyingine za afya kwa sababu wasipofanya hivyo watakuwa na majengo mazuri ya zahanati, vituo vya afya na hospitali lakini hakutakuwa na wataalam wa kuendesha vituo hivyo.

Kampeni ya “Furaha Yangu” ilizinduliwa kitaifa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa mnamo tarehe 16 mwezi juni mwaka huu makao makuu ya nchi jijini Dodoma.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YAKABIDHI KADI ZA MATIBABU BURE KWA WAZEE MKALAMA

    June 15, 2025
  • SIKU YA MTOTO WA AFRIKA WILAYANI MKALAMA

    June 16, 2025
  • Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkalama Apongeza Ujenzi wa Zahanati ya Nkenke

    June 13, 2025
  • ZIARA YA KAMATI YA SIASA MKOA WA SINGIDA

    June 11, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.