Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali ametoa muda mwezi mmoja kwa watendaji wa vijiji, kata na walimu wakuu wa shule kuhakikisha wanatatua changamoto ya uhaba wa madawati.
Kauli hiyo ametoa Aprili 25,2024 wakati wa kikao cha tathimini ya Madawati katika shule zote wilayani Mkalama kilichofanyika katika ukumbi wa Sheketela na kuhudhuriwa na Wakuu Idara, watendaji wa Vijiji, Kata pamoja na walimu wakuu shule.
"Natoa kipindi cha mwezi mmoja kwa watendaji wa vijiji,kata, walimu wa kuu shule za msingi na sekondari kuhakikisha tatizo hili la madawati linakwisha" DC Machali
Mbali na hilo, Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe.Moses Machali amepiga marufuku kukodishwa kwa mashamba ya shule badala yake yatumike kulima chakula kwa ajili ya wanafunzi.
"Ardhi ya shule isikodishwe kwa mtu yeyote ile, limeni chakula kwa ajili ya watoto wa shule. Nisisikie hata mwalimu anajikodisha shamba la shule" Mhe. Moses Machali
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.