Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewataka wafanyabiashara wilayani Mkalama kuhakikisha wanakata Leseni za biashara kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza ikiwa mfanyabiashara atabainiaka anafanya biashara bila ya kuwa na leseni.
Kauli hiyo ameitoa Juni 3,2024 wakati wa Kikao cha Baraza la Biashara kilichofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mkalama na kuhudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali pamoja na wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Halmashauri.
“Suala la leseni za biashara ni suala la lazima, tukate leseni za biashara ili tusije kukutana na adhabu mbalimbali. Tulipe kodi na ushuru kwa maendeleo ya wilaya yetu na kwa taifa kwa ujumla” Mhe. Moses Machali
Aidha Mhe. Moses Machali amewataka wafanyabishara kuhakikisha wanajiandikisha kupata namba ya NIDA ili kuweza kupata leseni kwa ajili ya kufanya biashara pamoja na shughuli mbalimbali zinahitaji kitambulisho cha NIDA.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Bi.Asia Messos amewaomba wafanyabishara na wananchi kwa ujumla wilayani Mkalama kujitokeza kuwekeza katika kiwanda cha kuchakata Nyanya kilichopo kata ya Gumanga wilayani Mkalama.
“Ningependa kutoa wito kwa wafanyabiashara kuja kuwekeza katika kiwanda hiki, tayari tupo katika mpango wa kuweka mashine mpya za kisasa. Wananchi, wafanyabiashara wote mnakaribishwa” DED Asia Messos
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.