Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali amewataka vijana wilayani Mkalama kupinga vikali vitendo vya ufisadi katika jamii kwa ustawi bora wa jamii na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo ameitoa Aprili 26/2024 katika viwanja vya shule ya sekondari Tumuli wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo kiwilaya yamefanyika katika shule ya sekondari Tumuli kata ya Tumuli wilayani Mkalama
“Waasisi wa Muungano wetu walikataa ufisadi na walichukizwa na vitendo vya ufisadi, ukimuona mtu ameiba mali ya umma au mali ya mtu mwingine mwambie haikubaliki” Mhe. Moses Machali
“Wazee wetu hawakupenda kusikia matendo mabaya kwa watoto, kwa watu wazima, kwa wazee na mtu yeyote, wazee wetu walianzisha muungano ili tupandeni, siku hizi upendo unapungua,natoa wito kwenu mmpendane” Mhr. Moses Machali
Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Mkalama, Ndugu Peter Masindi amewakumbusha wanafunzi hao kushikilia elimu kwa manufaa ya Maisha yao ya baadae sambamba na kuenzi Muungano.
“Maisha haya ni muungano, msome sana kwa bidii, muache utoro, mpende sana shule, maisha yenu ni mazuri” Peter Masindi, katibu Tawala wilaya ya Mkalama.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.