Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Mkalama, ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mhe. Moses Machali, leo Disemba 12 , 2023 imetembelea na kukagua miradi ya maji inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita katika vijiji vya Mwangeza , Kitongoji cha Gambasimboi Kata ya Mwangeza , Nkalakala pamoja na Mbigigi Kata ya Kikhonda ambapo kamati hiyo imefurahishwa na utekelezwa wa miradi hiyo.
Akiongea mara baada ya kumaliza kukagua miradi hiyo Mhe. Moses Machali ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuwezesha wananchi wa vijiji hivyo kupata maji safi na salama.
“Leo tumekagakua miradi mitatu, mradi wa kwanza ni mradi wa Gambasimboi wenye thamani ya shilingi milioni 109, baada ya hapo tulikwenda katika kijiji cha Nkalakala kutembelea mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 370 ambapo vitongoji 5 vitanufaika na mradi huu,tumetembelea pia mradi wa maji wa Mbigigi wenye thamani ya shilingi milioni 396, mradi huu unafadhiliwa na mfuko wa maji wa Taifa, ‘National Water Fund’ tunaishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt.Rais Samia Suluhu sasa wananchi wa maeneo haya watapata maji”, Aliongeza Mhe. Machali.
Akiongea kwa niaba ya wananchi diwani wa Kata ya Nkalakala Mhe.Athumani Jabili ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa Rais, Dkt .Samia Suluhu Hassan kupeleka mradi wa maji katika kijiji cha Nkalakala ambapo ameeleza kuwa mradi huo utakapokamilika utasaidia kupunguza magonjwa ya mlipuko kwani wananchi walikuwa wanatumia maji yasiyo salama ambayo walikuwa wanachota kwenye madimbwi.
“Tunaishukuru serikali kwa kuteletea mradi huu mzuri,Maji tumeyapokea kwa mikono miwili, tunamuomba Mungu mradi ukamilike ili wananchi wangu watumie kwa wema na pia kuondoa adha ya kuchota maji mbali yasiyo salama” Aliongeza Mhe. Jabili
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.