kamati ya Siasa Wilaya imetembelea na kukagua miradi ya maendeleo Wilayani Mkalama ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025.
Akiongea katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali ameitaka Idara ya Miundo mbinu na ujenzi Pamoja na kitengo cha manunuzi kuhakikisha wanasimamia kikamilifu miradi hiyo Pamoja na kitengo cha manunuzi kusimamia sheria ya manunuzi kwa Umma kulingana na bei iliyopo sokoni.
Pamoja na hayo Mhe. Machali aliwaagiza kuhakikisha wanaanda taarifa ya miradi yote iliyotembelewa na kukaguliwa na kamati ya siasa Wilaya kuainisha matumizi na gharama za miradi husika Pamoja na ramani za miradi hiyo na kuwasilisha ofisini kwake ndani ya siku tatu.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkalama Bw. Lameck Itungi amewataka wote wanaohusika na usimamizi wa miradi kusimamia kwa umakini ili uhalisia wa pesa uendane na thamani za utekelezaji na kuwaonya kuwa hawata wavumilia watendaji wabadhilifu watakaobainika kuhujumu miradi ambayo serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwaajili ya maendeleleo ya wananchi.
Miradi iliyotembelewa leo hii May 2, 2023 ni Pamoja na Jengo la dharula na Mochwari katika Hospitali ya Wilaya kata ya Nduguti ambayo yamegharimu Tsh 300,000,000 , ujenzi wa Nyumba ya Mkurugenzi Mtendaji Tsh 300,000,000, ujenzi wa Kituo cha Afya Ilunda Tsh 500,000,000, ujenzi wa daraja la Ndurumo linalounganisha vijiji vya Nkungi na Mng’anda Tsh18,500,000.
Miradi mingine iliyotembelewa ni Mradi wa maji Kinampundu utakaokuwa na vituo 12 vya kuchotea maji na utagharimu kiasi cha Tsh430,000,000, ujenzi wa zahanati ya Kenke 50,000,000 pamoja na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Kisubiu Tsh 470,000,000.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.