Kamati ya siasa Mkoa wa Singida ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa , Martha Mlata imetembelea na kukagua miradi mitatu yenye thamani ya Tsh.575,824,000/=katika Kata za Gumanga Kijiji cha Gumanga na Kata ya Nduguti Kijiji cha Nduguti.
Ziara hiyo imefanyika February 17, 2023 ambapo wametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Madarasa mawili Shule ya awali ya Mfano na matundu sita ya Vyoo katika Shule ya Msingi Gumanga uliogharimu kiasi cha Tsh. 55,824,000/=, Ujenzi wa Kituo cha Afya Gumanga chenye thamani ya Tsh.500,000,000 pamoja na kukagua kikundi cha Tunza Nduguti kinachojihusisha na ufugaji wa Ng’ombe wa maziwa na kilimo cha mahindi wenye thamani ya Tsh 20,000,000/=
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Mhe. Martha Mlata ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Mkalama kwa usimamizi mzuri wa miradi yote waliyotembelea Wilayani hapa na kuongeza kuwa miradi imezingatia ubora na fedha zilizotumika zinaendana na thamani ya miradi.
‘’Nimefurahishwa na namna ya utekelezaji wa miradi wilayani hapa ni tofauti na sehemu nyingine zote nilizopita, hii inatokana na ushirikiano mliouonyesha hapa leo, Mkurugenzi naona ofisi yako yote iko hapa pamoja na viongozi wengine Wilayani hapa hivyo naomba muendeleze ushirikiano huu ili muweze kufika mbali zaidi’’ Aliongeza Mlata mwenyekiti CCM Mkoa
Aidha Mhe. Mlata aliongeza kwa kusema kuwa ziara hiyo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi ya Mwaka 2020/ 2025 inayohakikisha inatoa fedha nyingi kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa masilahi mapana Nchi na kwa maendeleo ya Wananchi.
Katika hatua nyingine alifurahishwa na kikundi cha Tunza Nduguti chenye wanachama 10 waliopata mkopo wa Tsh. 20,000,000 kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama ambapo alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa usimamizi mzuri wa fedha hizo, ambapo alimtaka mkurugenzi kutenga fungu kwaajili ya Kikundi hicho Kwenda kujifunza ufugaji wa kisasa kupitia waliofanikiwa Zaidi ili kikundi hicho kiweze kuleta tija kwa familia zao na Wilaya ya kwa ujumla.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.