KAMATI YA FEDHA, MIPANGO NA UTAWALA HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA WAFANYA ZIARA YA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO
Kamati ya fedha ,Mipango na Utawala Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama leo Novemba 06 ,2023 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai-Septemba kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Baada ya kukagua na kutembelea miradi hiyo kamati iliongea na Wananchi wa Kijiji cha Kitumbili Kata ya Tumuli, Iguguno pamoja na Kikhonda ambapo wamesisitizwa kuunga juhudi ya Serikali ya awamu ya Sita kwa kuchangia shughuli za maendeleo ili iwe rahisi kwa Serikali kuwekeza katika maeneo yao.
"Serikali inaleta fedha nyingi kwaajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo Wilayani kwetu anzisheni Miradi ili Serikali iweze kuwa ‘Support’ aliyepo barabani ndiye anayepewa lift aliongea Mhe. Mkwega Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama"Mhe. Mkwega.
Mhe. mkwega aliwataka Watendaji kushirikiana na viongozi wa chama na Serikali kusimamia suala la Lishe Shuleni na kuwataka kuweka mkazo kwa wazazi ambao hawachangii chakula kuwepo kwa sheria zitakazowabana ili afua hiyo iweze kutekelezwa kwa Shule zote Wilayani hapa na watoto wapate chakula kwa kipindi chote wanapokuwa Shuleni.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na Kamati ya Fedha , Mipango na Utawala ni pamoja na Ujenzi wa daraja kijiji cha Kitumbili, Ukamilishaji wa Zahanati Kijiji cha Kitumbili,Ujenzi wa Kivuko cha Iguguno Shamba, Ukarabati wa Shule kongwe Shule ya Msingi Iguguno, Ukamilishaji wa Zahanati ya Lukomo , Ujenzi wa Maabara Shule ya Sekondari Kikhonda pamoja na ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Shule ya Irama.
Ziara hiyo itaendelea kesho Novemba 07,2023 katika Kata za Nduguti, Miganga pamoja na Msingi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.