Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali, leo ametangaza Oparesheni maalum ya kuwakamata wazazi, walezi wote wenye watoto waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza lakini bado hawajafika shule mpaka sasa..
Tamko hilo amelitoa Januari 17/2024 wakati wa kikao kazi na wakuu wa Idara, watendaji kata, vijiji, maafisa tarafa pamoja na wakuu wa shule kilichofanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo katika halmashauri ya wilaya ya Mkalama.
"Kamata kila mzazi, mlezi mwenye mtoto aliyefaulu na hajajiunga kidato cha kwanza mpaka sasa. Mtu yeyote atakayekwamisha zoezi kamata.. Hata kama hawana sare wasome kwa muda wa mwezi mmoja, nisisikie mwanafunzi kakataliwa kisa sare" Mhe. Moses Machali
"Kufikia Jumatatu, kama wanafunzi hawajafika shule, mtakula pingu wote Mtendaji wa Kata,Kijiji, Afisa Tarafa na Wakuu wa shule. Nisikikie kelele kuwa wananchi wanaonewa. Nataka watoto waende shule. Madiwani mnatakiwa kutuunga mkono” Mhe. Machali
Aidha Mhe.Machali amesema hadi kufikia Januari 25/2024 kila mtumishi awe anaishi katika kituo chake cha kazi kabla ya kuanza kwa oparesheni kali Januari 28/2024 ya kubaini watumishi watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo ili wachukulie hatua kali.
"Walimu, Maafisa Elimu Kata, Watendaji wa Vijiji, Kata, na Watumishi wa Afya, Waratibu wa Elimu wote muishi katika vituo vyenu vya kazi, tunawajibu wa kuleta mabadiliko katika vijiji. Hatuwezi kufika tunakotaka kufika. Tunataka kazi ifanyike" Mhe Moses Machali
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.