• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

Juma la Elimu lafana Mkalama

Imewekwa kwenye: May 14th, 2018

Wilaya ya Mkalama leo imeingia katika moja ya rekodi za Kitaifa baada ya kufungua rasmi maadhimisho ya juma la Elimu kwa mwaka huu.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ya kitaifa mwaka huu alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Daktari Rehema Nchimbi ambapo pamoja na mambo mengine alitumia hotuba yake kusisitiza Mtandao wa Elimu kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na serikali katika sekta hiyo.

“Kauli mbiu yenu ya uwajibikaji wa pamoja katika kuinua elimu nchini inapaswa kutekelezwa kwa vitendo na jamii yote ya Mkalama kwa sababu sioni sababu ya wazazi wa wanafunzi wa Mkalama kushindwa kuchangia chakula cha watoto wao shuleni wakati nina ushahidi kuwa wazazi hawa ni wakulima wazuri” Aliongeza  Mhe. Nchimbi.

Mhe. Nchimbi aliwataka wananchi watumie vizuri mbegu za pamba na korosho walizopewa na serikali bila malipo yoyote kuhakikisha wanapata mavuno mengi yatakayowasaidia kuchangia elimu.

“Kuanzia sasa ninaagiza shule zote za sekondari hapa Singida ni lazima ziwe na mabwawa ya kufuga samaki ambapo mbali na kupata chakula kupitia mabwawa hayo pia kitakuwa ni chanzo kizuri cha mapato kwa kila shule kwa sababu soko la samaki ni kubwa sana hasa Mkoa jirani wa Dodoma, mtapata, hili sio ombi ni lazima! Alisisitiza Mhe. Nchimbi.

Mhe. Nchimbi aliwaagiza wakurugenzi wote wa Halmashauri zilizopo Mkoani Singida kuhakikisha wanampa taarifa za utekelezaji wa agizo hilo kila ifikapo mwisho wa Mwezi  na taarifa hizo  apatiwe moja kwa moja katika ofisi yake.

“Tunawashukuru sana TenMet kwa kutuandalia juma hili na tunawaahidi haya mema yote mliyotupa tutayarudisha kwa mema pia na kwa mchango Mkubwa ambao serikali ya awamu ya tano imetoa katika Elimu ya Mkalama hatuwezi kubaki nyuma tena na safari hii tunataka kama tukiwa wa mwisho basi tuwe wa mwisho kwa ufaulu wa asilimia 90” Alimalizia Mhe. Nchimbi.

Wakati huo huo  Wilaya ya Mkalama ilipata ugeni wa ziara ya muda mfupi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo ambaye alifika kwa ajili ya kukagua thamani ya fedha kulingana na ubora wa jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ambapo aliridhika na kazi iliyofanyika  kwa awamu ya kwanza na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhandisi Gofrey Sanga kuhakikisha viwango hivyo vya ubora vinazingatiwa katika ujenzi wa awamu ya pili ya Ofisi ya hiyo.

“Mkalama ni moja ya Wilaya change hivyo inahitaji kupewa kipaumbele katika miradi mbalimbali na nikuhakikishie Mhe. Mkuu wa Mkoa, Wizara yangu itahakikisha Mkoa wa Singida kwa ujumla unasonga mbele” Aliongeza Mhe. Jafo.

Mhe. Jafo pia alisema kuwa mbali na kujenga vituo viwili vya Afya vya Kisasa ambavyo ni Kinyambuli na Mkalama, Kwa Mkoa wa Singida serikali ya awamu ya tano imetenga fedha za ujenzi wa hospitali mbili za Wilaya ambazo zitajengwa katika Wilaya ya Mkalama na Singida vijijini.

“Naomba nitumie fursa hii kukutamkia wazi Mkuu wa Mkoa na wananchi wote wa Singida vijijini kwa ujumla kuwa hospitali ya Wilaya Singida Vijijini itajengwa Ilongelo na sitaki mtu yoyote ahangaike kuja ofisini kwangu kujadili juu ya hilo, mimi nimeshalimaliza kwa sababu nachoangalia mimi ni kupeleka hospitali sehemu ambayo nina uhakika wananchi wengi zaidi watapata huduma na sio kundi la watu wachache wanaojaribu kuangalia maslahi yao kisiasa” Alimalizia Mhe. Jafo.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.