Jamii imetakiwa kujitathimini juu ya maadili na malezi kwa watoto kwakuweka msawazo wa ratiba za kazi na malezi ya familia ambayo yamebainika kuwa changamoto kwa watoto nakupelekea kuiiga tamaduni za kimagharibi zinazochochea kushuka kwa maadili.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Moses Machali ameyasema hayo mapema leo May 15, 2023 wakati akifungua kongamano la siku ya familia lilifanyika katika ukumbi wa Sheketela uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
Aidha Mhe. Machali ameongeza kuwa Kila mmoja ni kiongozi mahala popote anowajibu wa kulinda mambo yote mema na kuwafundisha watoto kuwa na maadili mema ili kutengeneza taifa lenye maadili mazuri kwa maslahi mapana ya Wilaya na Taifa kwaujumla.
‘’familia nyingi za Kitanzania zinakabiliwa na changamoto nyingi zinazopelekea wazazi kuwa ‘busy ‘ na kazi zao na kusahau jukumu la kulea familia , sikatai mtu kufanya kazi lakini wazazi tunaowajibu wa ‘kubalance ‘ kazi na malezi ili watoto wetu wabaki salama kwa masilahi mapana ya Taifa hili’’Aliongeza Mhe Machali.
Aliendelea kwakusema kuwa wazazi kwakushirikiana na walimu wanalojukumu kubwa la kuendeleza malezi mazuri pamoja na kukemea wazi wazi vitendo vyote vya kihalifu kama vile ushoga na usagaji ili taifa lipone na kuwa na kizazi chenye hofu ya Mungu.
Pamoja na hayo amewataka wananchi kutumia siku ya leo kutafakari mienendo yao juu ya malezi ya familia na kuunda familia mpya ambayo italeta matokeo chanya kwa kizazi kijacho.
Afisa maendeleo ya jamii Bw. Mohamed Atiki amesema Wilaya ya Mkalama imeungana na Nchi uanachama za umoja wa Mataifa kuadhimisha siku ya familia ambayo hufanyika Mei 15 kila mwaka ikiwa na lengo la kutoa kipaumbele cha kujadili mambo mbalimbali yahusuyo familia na jamii.
Bw. Atiki ameongeza kuwa siku hii muhimu hutoa fursa ya kujadili masuala yanayoathiri familia ikiwemo kijamii, kiuchumi na hata kidemografia ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima inayopelekea familia nyingi kusambaratika na kuacha watoto bila uangalizi wa pamoja na kukosa huduma muhimu.
Pamoja na hayo amesema kuwa ushindani uliopo katika soko huria ni changamoto kwa kizazi cha sasa kutopata muda wa kutosha wa kuwa na familia na kutoa wito kwa Wananchi wote kushiriki kikamilifu katika katika malezi ya watoto.
‘’Imarisha maadili na upendo kwa familia Imara‘’hii ndio kauli mbiu ya siku ya familia leo May 15, 2023.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.