Jamii imetakiwa kukosemesha na kukemea vitendo vyote dhidhi ya ukatili kwa wanawake na Watoto wa kike ili kuleta usawa wa kijinsia na kuhakikisha wanawake wanapewa haki katika nyadhifa mbalimbali za uongozi .
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe, Moses Machali ameyasema hayo March 8, 2023 katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani ambayo Wilayani Mkalama yamefanyika katika Kijiji cha Singa kilichopo Kata ya Kinampundu.
‘’ Ni ushamba na ni ujinga kuona wanaume wanawanyanyasa wanawake katika jamii wakati tumeona wanawake wanaonyesha uwezo Mkubwa katika Nyanja mbalimbali za uongozi kama tunavyoona Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Mwanamke, na wengine wengi hata hapa Wilayani tunaona DAS wetu ni mwanamke, Mkurugenzi ni mwanamke na wengine wengi , tena wana michango na mawazo mazuri kuliko hata sisi wanaume ambayo yanaleta tija kwa jamii’’ Alisisitiza Mhe. Machali
Aidha Mhe. Machali aliongeza kuwa siku hii Adhimu ya wanawake Duniani ikalete chachu kwa jamii kumheshimu mtoto wa kike na kumpatia haki ya Elimu na wanawake wote kwa ujumla huku akisema kwa yeyote atakayebainika kufanya vitendo vya kikatili kwa wanawake Wilayani hapa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mhe. Machali amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka 2023 ni ’Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia chachu katika kuleta usawa wa kijinsia’ ikalete mabadiliko na usawa wa kijinsia katika jamii huku akiitaka jamii kutumia vizuri mabadiliko hayo kujenga jamii yenye usawa inayotenda haki kwa masilahi mapana ya kizazi kijacho.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.