• Wasiliana nasi
    • Maswali
    • Barua Pepe
    • Malalamiko
Mkalama District Council
Mkalama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Utawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Takwimu
      • Kilimo na Ushirika
      • Mifugo
      • Usimamizi wa Mazingira
      • Biashara na Fedha
      • Afya
      • Ardhi na Mipango ya Mji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Miundombinu
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Kisheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi, Ugavi & Vifaa
      • TASAF
      • Biashara
  • Fursa za Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Mfumo wa Taarifa za Shule Tanzania
    • Uvuvi
    • Sekta ya Huduma
    • Ardhi iliyotengwa kwaajili ya Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma ya kwanza
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha Utawala na Mipango
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao vya Kisheria
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
      • mwongozo kutoka Tamisemi
      • uongozi ngazi ya vijiji
      • vibali vya ujenzi
      • mfumo wa anwani za makazi
    • Ripoti
      • Taarifa ya CAG 2018
    • Sheria
      • sheria ya fedha
    • mkataba
    • Fomu za Maombi kwa Wateja
      • Leseni ya biashara
      • maombi ya kiwanja
      • leseni za vileo
    • Sera
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
      • Pongezi
      • Matokeo ya Uchaguzi Kinampundu
      • KURUDISHWA KAZINI
      • Juma la elimu
    • Video
    • Hotuba
    • Picha
    • Habari
    • Matukio

IRAMBA YAIADHIBU MKALAMA

Imewekwa kwenye: April 13th, 2018

Jioni ya leo katika Wilaya ya Mkalama imewekwa historia baada ya kuchezwa mchezo wa mpira wa Miguu kati ya timu ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama na timu ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba huku kikosi cha timu ya Iramba kikiongozwa na Waziri wa mambo ya ndani Mhe. Mwigulu Nchemba.

Katika Mchezo huo uliomalizika kwa timu ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kufungwa jumla ya magoli 3-1 kulikuwa na vivutio mbalimbali huku burudani kubwa ikiwa ni kiwango kizuri kilichokuwa kikioneshwa na Mhe. Nchemba na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga ambaye ndiye alikuwa mfungaji wa bao pekee la timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.

Timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ilianza kuhesabu kalamu yake ya magoli kupitia kwa Mshambuliaji wake tishio katika mcheo wa leo Mhe. Mwigulu Nchemba ambaye alifunga goli hilo baada ya kuachia shuti kali kufuatia mpira uliompita beki wa timu ya Mkalama John Tibu.

Zikiwa zimesalia dakika chache kabla ya kuelekea mapumziko, Kiungo wa timu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mhandisi Godfrey Sanga aliisawazishia timu yake goli baada ya kukwamisha kiufundi wavuni penati yake iliyotokana na beki wa timu ya Iramba kuunawa mpira wakati akiwa kwenye heka heka za kuokoa mpira uliopigwa na Mshambuliaji Lunzegere Kilala.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, timu hizo zilikuwa zimetoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bao 1-1.

Maelekezo ya walimu wa timu zote mbili wakati wa mapumziko yalionekana kuzaa matunda zaidi upande wa timu ya Iramba baada ya kufanikiwa kupachika goli la pili kupitia kwa Mhe. Mwigulu Nchemba kwa mara nyingine tena huku safari hii akifunga goli hilo baada ya “piga nikupige” zilizotokea katika goli la timu ya Mkalama.

Mara baada ya kufungwa goli la 3 lililofungwa dakika 10 tu baada ya goli la pili, timu ya Mkalama ilifanya mabadiliko ya wachezaji hatua ambayo yalionesha mafanikio baada ya timu hiyo kuongeza kasi ya mashambulizi lakini hata hivyo kasi hiyo haikuweza kuzaa matunda kutokana na uhodari uliooneshwa na kipa wa timu ya Iramba ambaye alipangua michomo kadhaa iliyokuwa ikielekezwa golini kwake.

Mara baada ya kumalizika kwa Mchezo, Nyota wa mchezo huo ambaye pia ni  Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mhe. Mwigulu Nchemba aliushukuru Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kwa maandalizi mazuri ya tukio hilo huku akiomba jambo hilo liwe endelevu.

“Mimi na Mhe. Kiula tukiwa bungeni huwa tunashughulikia changamoto zetu kwa pamoja kwa sababu kwetu Iramba ni moja hivyo ni vizuri ushirikiano huu tuuenzi na kuudumisha” Aliongeza Mhe. Nchemba.

Akijibu ombi fupi lililowasilishwa na Mbunge wa jimbo la Mkalama Mhe. Allan Kiula kuhusu umaliziwaji wa kituo cha polisi kilichopo Nduguti, Mhe. Nchemba alisema kuwa katika bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani inayotarajiwa kusomwa tarehe 30  mwezi huu, kipaumbele cha Ujenzi na uboreshaji wa vituo vya polisi  kimewekwa Wilaya mpya zote ikiwemo Wilaya ya Mkalama.

“Lakini pia ombi la Mhe. Kiula la kutaka timu ya madiwani wa Halmashauri zote mbili za Iramba na Mkalama kucheza na timu ya bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepita hivyo tutakaa na Mhe. Kiula na kupanga tarehe rasmi ya mechi hiyo” Alisisitiza Mhe. Nchemba.

Mchezo huo ulitanguliwa na Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama robo ya pili uliofanyika mapema asubuhi ambapo kamati mbalimbali ziliwasilisha taarifa zao na waheshimiwa madiwani kupata nafasi ya kuuliza maswali ya papo kwa hapo kwa Wenyeviti wa kamati hizo, Mkurugenzi na Wataalam mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAHILI KUANZIA TAREHE 09-10-2024 HADI 14-10-2024 October 03, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI WA AFYA MKALAMA WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

    April 24, 2025
  • WANAWAKE MKALAMA WAHIMIZWA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

    March 06, 2025
  • DC MACHALI ATOA WITO WATU WA AFYA MKALAMA KUFANYA KAZI KWA BIDII

    February 19, 2025
  • SEMINA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI MKALAMA

    February 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Taarifa ya fainali kati ya Kisuluiga na Nkungi
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • eMrejesho -Tuma Malalamiko, Maoni au Pongezi
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja

Viungo vinavyohusiana

  • Utumishi
  • Tovuti ya Ikulu
  • TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Idara ya Habari Maelezo
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582

    Anuani ya Posta: P.o. Box 1007

    Simu ya Mezani: 026-2964005

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.