Bi Messos amesema kuwa kupitia mradi wa Boost Halmashauri imepokea na kutumia jumla ya shilingi Tsh. 925,400,000 katika ujenzi wa shule moja mpya ya Msingi (Shule ya Msingi Nkindiko),Jengo 1 la utawala,Nyumba 1 ya Mwalimu,Madarasa 56,Matundu ya vyoo 42,Madawati 405, pamoja na kupokea kiasi cha Tsh. 238,000,000 kwaajili ya ukarabati wa shule Kongwe 11 za Msingi.
Kupitia mradi wa SEQUIP Halmashauri imepokea jumla ya Tsh. 544,225,626 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari (Mkalama One) na Tsh. 110,000,000 kwaajili ya ujenzi wa nyumba mpya ya mwalimu katika shule ya Sekondari Kisubiu.
Aidha Bi. Messos ameongeza Kwa kusema kuwa Halmashauri kupitia mapato ya ndani katika sekta ya elimu pekee imepeleka jumla ya Tsh. 47,500,000 ambapo zimetumika katika ukamilishaji wa Maabara Shule ya Sekondari Tumuli Tsh. 12,500,000, Ujenzi wa darasa 1 shule ya Msingi Maelu 23,000,000, Ukamilishaji wa darasa 1 shule ya Msingi Kinandili
“Ujenzi wa miundombinu yote umeshakamilika pamoja na usajili wa shule mpya mbili. Halmashauri ipo tayari kuwapokea wanafunzi wapya wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza ifikapo Januari, 2024”, ameongeza Bi. Messos.
Sambamba na hayo ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais msikivu Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kutoa pesa hizo kwaajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo Wilayani hapa nakusema kuwa Kila pesa itakayokuja kwaajili ya miradi itasimamiwa kikamili na kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
@ded_mkalama @ofisi_ya_rais_tamisemi @omaryksadick @joramnabaili
#mkalamasalamakaziiendelee
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.