Na Rachel Joram
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Binilith Mahenge ameipongeza Halmashauri ya wilaya wa Mkalama kwakutekeleza takwa la kisheria la kutoa 10% yamapato yake ya ndani kwaajili ya mikopo kwa Vikundi vya vijana , wanawake na walemavu.
Ameyasema hayo mapema leo wakati akikabidhi kiasi cha Tsh. 2,000,000 kwa kikundi cha Vijana cha Iguguno (IGUGUNO YOUTH GROUP) katika Kijiji cha Iguguno kata ya Iguguno ikiwa ni kutimiza ahadi yake aliyoahidi hivi karibuni ikiwa ni kuunga Mkono juhudi za Halmashauri inayotenga 10%kwa makundi ya vijana ,wanawake pamoja na watu wenye ulemavu.
Pamoja na pongezi hizo amewataka viongozi wa Halmashauri kusimamia vikundi vinavyopata mikopo ili kuona ni vikundi gani vinafanya vizuri.
‘’haitaleta maana kama Halmashauri inatoa shilingi milioni kumi na tano na kikundi kinakufa, Halmashauri kuna wataalamu wengi kama vile Afisa maendeleo ya jamii na wahandisi na hizi kazi zakufyatua tofali ni za kihandisi hivyo tunatarajia tofali zinazofyatuliwa na kikundi hiki ziwe bora na kuwa na soko kuliko tofali za kikundi kingine chochote kwasababu halmashauri imewekeza kwenu na inawataalamu wengi kuweza kushauri vikundi hivyo’’Aliongeza RC Mahenge.
Hata hivyo amewataka wanakikundi hao kuwatumia wataalamu kwa kazi wanazofanya ili kupata uelewa na ujuzi Zaidi kutoka kwa wataalamu mbalimbali na kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi Zaidi na ubora.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Mheshima Sophia Mfaume Kizigo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kuwaunga mkono na kuongeza kuwa kitendo hicho kitawatia moyo wanakikundi hao kwani viongozi wanatambua wanachokifanya na kuwa chachu ya maendeleo yakikundi hicho kwakufanya kazi kwa ufanisi Zaidi ambapo ameahidi kuwa uongozi wa wilaya ya Mkalama watasimamia vikundi hivyo vyema na kurejesha fedha hizo kwa wakati ili kunufaisha vikundi vingine vilivyopo ndani ya wilaya ya Mkalama.
Kwa upande wake Mwenyekiti wakikundi hicho Bi. Vick Mwisakila amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwakufika nakujionea shughuli za kikundi hicho na kusema kuwa fedha hizo alizowachangia watafanya jambo kubwa katika kikundi hicho pia ametumia fursa hiyo kuwakaribisha vijana wengine kujiunga kwenye vikundi na kuacha Imani za kusubiri ajira serikalin
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.