Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Sophia Kizigo ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kuhakikisha Kila baada ya miezi mitatu (3) vikao vya kamati za Watu wenye Ulemavu na Baraza la Wazee linakaa kujadili mambo mbalimbali yanayowahusu Wazee na Walemavu kwa masilahi mapana ya makundi haya.
Ametoa maagizo hayo wakati akizindua Kamati ya Watu wenye ulemavu na Baraza la Wazee ngazi ya Halmashauri lililofanyika mapema leo katika Ukumbi wa Sheketela uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.
Aidha, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya inasisitiza uwepo wa kamati za Watu wenye ulemavu na Mabaraza ya Wazee kuanzia ngazi ya Taifa hadi Mitaa / Vijiji hivyo kuwepo kwa vikao vya mara kwa mara vitarahisisha wajumbe kusimamia upatikanaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu katika mazingira jumuishi bila ubaguzi katika nyanja zote.
Pamoja na hayo aliwataka Wajumbe wa Mabaraza hayo kila mmoja kwa nafasi yake kusimamia majukumu yake huku akiutaka uongozi wa Baraza la Wazee kuhakikisha wanaishauri na kuishawishi Serikali na wanasiasa kuboresha huduma kwa Wazee na wategemezi wao .
Akitoa neno la shukrani kwaniaba ya wajumbe hao Magreth Kinota aliupongeza uongozi wa Wilaya ya Mkalama kwa kazi nyingi zenye masilahi mapana kwa jamii ambapo aliahidi watafanya kazi kwaushirikiano ikiwa ni pamoja na kulinda na kukuza ustawi na Maendeleo ya watu wenye ulemavu kama vile kupewa mikopo ya asilimia mbili pamoja na kuishawishi Serikali kutoa vitambulisho kwa Wazee wenye miaka sitini (60) na kuendelea kwaajili ya kupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo afya, Maji pamoja na kupata msamaha wa kodi za majengo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.