"HAKIKISHENI MNASIMAMIA MIRADI YENU VIZURI” -DED ASIA MESSOS
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkalama Bi Asia Messos amewataka watendaji wa vjiji,kata wenye miradi kuhakikisha wanasimamia vizuri miradi yao pamoja na kuweka bajeti nzuri ili kuepukana na tatizo la miradi kutokamilika kwa wakati.
Agizo hilo amelitoa Januari 12,2024 wakati wa kupokea taarifa ya vijiji vitakavyopokea fedha ya jimbo kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo inayotokelezwa katika vijiji, kata husika katika Halmashauri ya wilaya ya Mkalama iliyowasilishwa na Afisa Mipango katika ukumbi wa Sheketela uliopo wilayani Mkalama.
" Kila mwenye mradi asimamie mradi wake mpaka ukamilike. Tuzingatie bajeti, umepokea pesa kaa chini fanya tathimini kulingana na bajeti uliyopewa. Hii itatusaidia tuondokane na tatizo la miradi kutokukamilika. Ukiona mradi unachangamoto yeyote tuambiane.” Amesema Bi Asia Messos
Pia Mkuregenzi Mtendaji Bi Asia Messos amewataka watendaji kuhakikisha wanazingatia hali ya usafi katika miradi yao pamoja na kuwataka walimu ambao shule zao hazina umeme walete orodha ya shule hizo ofisini kwa ajili ya kutatua changamoto hiyo.
Awali, akiwasilisha taarifa ya orodha ya vijiji vitakavyonufaika na fedha za jimbo kwa mwaka wa fedha 2023/24, Afisa Mipango wilaya ya Mkalama Ndugu James George Paul amesema jumla ya fedha Tsh milioni 72,995,000 zitapelekewa katika vijiji 13 kwa ajili ya kukamlisha miradi mbalimbali ya afya na elimu inayotekelezwa na serikali katika vijiji hivyo.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.