Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhe. Mosses Machali ameutaka uongozi wa Jumuiya za watumia maji Kijiji cha Kidarafa, Kata ya Mwaga kutumia mapato wanayopata kuongeza vituo vya kuchota maji ili kusogeza huduma kwa wananchi katika kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma hiyo.
Amesema hayo mapema leo Machi 14, 2024 wakati akisikiliza na kutatua kero za wananchi wa kijiji cha Kidarafa na Kidigida katika mikutano ya hadhara iliyofanyika kwa nayakati tofauti tofauti katoka kata ya Mwanga Wilayani Mkalama.
Aidha amewaomba wananchi kuendelea kuunga mkono serikali ya awamu ya Sita kwani imedhamiria kutatua changamoto mbalimbali katika Sekta ya Maji, Nishati ya Umeme, Barabara, Afya pamoja na Elimu ndio maana inahakikisha inafikisha huduma hadi kwenye ngazi ya vitongoji.
‘’Ninawaomba wananchi tuendelee kuunga mkono serikali iliyopo madarakani, nani alitegemea kama umeme ungefika kidigida, nani alitegemea leo maji kidarafa yangepatikana kwa wingi namna hii? Hii inatokana na Serikali imara iliyopo madarakan’’. aliongeza Dc Machali.
Pamoja na hayo aliwataka wananchi katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuchagua viongozi watakaokidhi mahitaji yao na kuacha kuchagua viongozi wenye maslahi yao binafsi huku akiwataka viongozi wanaotajwa kuhujumu juhudi za Serikali kujisahihisha na kujitafakari kabla ya uchaguzi.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.