Elimu ya ukatili wa kijinsia imeendelewa kutolewa katika nyaja mbalimbali ikiwepo shuleni ambapo watoto wanafanyiwa vitendo vya kikatili na kutishiwa kusema huku vikiendelea kuwaacha na matatizo makubwa katika miili yao akili pamoja na kuwaharibu kihisia watoto hao.
Gladness Msemwa kutoka Wizara ya katiba na sheria amesema hayo wakati akitoa elimu ya masuala ya haki za watoto pamoja na ukatili wa kijinsia katika Shule ya Sekondari Nkinto na Shule ya Msingi Makulo Kata ya Nkinto Wilayani Mkalama.
Aidha aliwataka watoto kutambua haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na haki ya kuishi, haki ya kupata elimu, kuendelezwa pamoja na haki ya kulindwa huku akiwasihi kutoa taarifa pale wanapohisi kuna viashiria au vitendo vya ukatili katika familia, jamii na hata shuleni.
‘’Kuna wengine mnafanyiwa ukatili majumbani mwenu, shuleni na hata kwenye jamii au ndugu wa karibu lakini mnaogopa kutoa taarifa unajikuta kama ni mtoto wa kiume unalaitiwa hadi unaharibika sawa na watoto wa kike inapelekea kuathirika ’kisaikoloji’ lakini hamsemi ili msaidiwe kwakuhofia kuuliwa au kwa vile anakupa vizawadi ’’ Aliongeza Msemwa.
Pamoja na hayo Msemwa aliwataka wazazi kujenga urafiki na watoto ili kujua maendeleo yao au kuwaambia mambo wanayofanyiwa pia kuhakikisha wazazi wanawalinda watoto wao dhidi ya vitendo vya kikatili na kuacha kumaliza kesi nyumbani inapobainika mtoto kafanyiwa ukatili na ndugu wa karibu na familia kwani kwakufanya hivyo wanaendelea kulea na kukumbatia waovu wanaoharibu taifa la kesho.
Musa Christopher pamoja na Naomi Matemanga wanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Nkinto wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Mama Samia Legal Aid Compaign) kufika shuleni kwao na kutoa elimu juu ya masuala ya haki za watoto pamoja na ukatili wa kijinsia ambapo wamesema watatumia elimu waliyoipata kuibua vitendo vya kikatili kwenye maeneo yao pamoja na kuwa mabalozi wazuri kwa wengine.
OFISI YA MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MKALAMA, 18 MASAKA RD, 43582
Anuani ya Posta: P.o. Box 1007
Simu ya Mezani: 026-2964005
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ded@mkalamadc.go.tz
Copyright ©2018 Mkalama DC . All rights reserved.